BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) linatarajiwa kupiga kura ya kuidhinisha jeshi la kulinda usalama nchini Somalia kuongezwa kwa zaidi ya wanajeshi 5,000. Taarifa zaidi zinasema, hali hiyo itafanya idadi ya wanajeshi wote wa kuhifadhi amani walio Somalia kufikia 17,731. Hadi sasa kuna jumla ya wanajeshi 12,000 wa kigeni nchini humo.
Kura hiyo ya Baraza la Usalama kutaipa fursa jeshi la Kenya ambalo kwa sasa liko nchini Somalia likipambana na Al shabaab, nafasi ya kupigana chini ya mwamvuli wa Jeshi la Umoja wa Afrika. Upigaji huo wa kura unakuja siku moja tu kabla ya kuanza kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia mjini London.
Katika kura hiyo itakayo pigwa hii leo, biashara ya kuuza makaa ambayo ndio njia kuu ya kundi la Al Shabaab kujipatia pesa, itaharamishwa marufuku. Kundi hilo la Al Shabaab kwa wakati huu linamiliki sehemu nyingi za kusini mwa Somalia ambayo tangu mwaka wa 1991 zimekuwa hazitawaliwi na serrikali ya Kuu.
Katika kipindi hicho cha karibu miongo miwili, wasomali zaidi ya milioni moja na nusu wamehama nchi kufuatia machafuko yasio malizika. Mwaka jana wapiganaji wa Al Shabaab walilazimika kuuhama mji wa Mogadishu kufuatia mashambulizi makali kutoka kwa yanayoendeshwa na wanajeshi wa umoja wa Afrika.
Mbali na kuweko majeshi ya Uganda, ya Djibouti na yale ya Burundi, wanajeshi wa Ethiopia pia wameingia nchini Somalia kupambana na Al Shabaab. Kwa hiyo mapendekezo ya ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utayapa majeshi yanayopigana chini ya mwamvuli wa Jeshi la Afrika fursa ya kuingia sehemu nyegine za Somalia. Hii lengo la kupunguza na hatimae kuondoa kabisa tisho la Al Shabaab nchini Somalia.
Upigaji huo wa kura unakuja siku moja tu kabla ya kuanza kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia mjini London. Katika kura hiyo itakayo pigwa hii leo , biashara ya kuuza makaa ambayo ndio njia kuu ya kundi la Al Shabaab kujipatia pesa, itaharamishwa marufuku.
Kundi hilo la Al Shabaab kwa wakati huu linamiliki sehemu nyingi za Kusini mwa Somalia ambayo tangu mwaka wa 1991 zimekuwa hazitawaliwi na serrikali ya Kuu. Katika kipindi hicho cha karibu miongo miwili, wasomali zaidi ya milioni moja na nusu wamehama nchi kufuatia machafuko yasio malizika.
Mwaka jana wapiganaji wa Al Shabaab walilazimika kuuhama mji wa Mogadishu kufuatia mashambulizi makali kutoka kwa yanayoendeshwa na wanajeshi wa umoja wa Afrika. Mbali na kuweko majeshi ya Uganda, Djibouti na ya Burundi, wanajeshi wa Ethiopia pia wameingia nchini Somalia kupambana na Al Shabaab.
Kwa hiyo mapendekezo ya ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utayapa majeshi yanayopigana chini ya mwamvuli wa jeshi la Afrika fursa ya kuingia sehemu nyegine za Somalia. Hii lengo la kupunguza na hatimae kuondoa kabisa tisho la Al Shabaab nchini Somalia.
-BBC