Wanafunzi Walioshinda Shindano la JATA Wazawadiwa

Washindi kumi walioshiriki shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo mshindi wa kwanza alipata laptop yenye thamani ya dola 600 za kimarekani. Picha na Anna Nkinda – Maelezo.

Meneja wa shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama Ali Mindria (kulia) akipokea kombe la ushindi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee kutoka kwa Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA). Wanafunzi wane kutoka shule hiyo waliingia kumi bora kwa kushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa kati ya wanafunzi 32 walioshiriki shindano hilo. Picha na Anna Nkinda – Maelezo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni na wanafunzi wanne kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama walioshiriki shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) nakushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo shule ya WAMA-Nakayama aliibuka mshindi wa jumla. Picha na Anna Nkinda – Maelezo