
Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo kwenye manispaa ya Dodoma wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) waliotembelea Shule hiyo Mchana wa leo

Mmoja wa Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akishusha Baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wakati wanafunzi wa UDOM walipowasili Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo Manispaa ya Dodoma Mjini mchana wa leo.

Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Areman Kaziguto (mwenye fulana nyeupe) akitoa maelezo machache mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya viwandani iliyopo Manispaa ya Dodoma mjini ambapo wanafunzi wa UDOM leo walifanya ziara na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia Usafi