Wanafunzi na Mwalimu Wao Wafa kwa Radi Kigoma

Mwalimu Veronika Mtes  wa Shule ya Msingi Kibirizi aliyepata mshtuko baada ya tukio la radi akiwa katika hospitali ya Mawenzi mkoa wa Kigoma kwa matibabu.

Mwalimu Veronika Mtes wa Shule ya Msingi Kibirizi aliyepata mshtuko baada ya tukio la radi akiwa katika hospitali ya Mawenzi mkoa wa Kigoma kwa matibabu.


Mwalimu Merina Sekilo aliyenusurika kupigwa na radi wakati akifundisha darasa la kwanza,ambapo wanafunzi 6 walifariki

Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Kigoma, Maweni akiongeza na Waandishi wa
habari juu ya tukio la radi lililotokea hivi punde na kuuwa watu 8

Na Editha Karlo Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

WATU
wanane wakiwemo wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi kibirizi
mmoja pamoja na mtu wa kawaida mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa
wamekufa baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengi 15 wakijeruhiwa
na radi hiyo mchana huu.

Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa kigoma(maweni)Dkt Fadhili Kabaya
alisema kuwa watu hao walifikwa na mauti hayo kufiatia mvua kubwa
zilizonyesha zikiambana na radi zilianza majira ya saa sita mchana.

Dkt
Fadhili aliwataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwalimu
wa shule ya msingi kibiriziElinaza Mbwambo(25)mtu mwingine wa kaida ni
Forcus Ntahaba(45)mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa.

Aliwataja
wanafunzi waliofariki ambao wote ni wa darasa la kwanza kuwa ni Yusuph
Ntahoma(8)Hassan Ally(9)Fatuma Sley(7)Zamda Seif(8)Shukranmi Yohana(7)
na Warupe Kapupa(10).

Alisema
walipokea majeruhi kumi na tano lakini kati yao kumi wametibiwa na
kuruhusiwa kurudi nyumba baada ya hali zao kuwa nzuri na watano
wamelazwa wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.

Akisimulia
tukio hilo mwalimu aliyekuwa anafundisha darasani Mwalimu Merina Sililo
alisema kuwa akiwa darasani akiendelea kufundisha ghafla aliona wingu
zito jeusi limetanda hadi akashindwa kuendelea kuandika ubaoni.

”Manyunyu
yalianza kidogo kidogo ikaja mvua kubwa na radi pamoja na miungurumo
mikali sana iliyopelekea wanafunzi kuanguka ovyo darasa na kuzima na
mara niliona moto umetanda katika chumba kuzima cha darasa na mimi
nilianguka chini na kupoteza fahamu”alisema mwalimu huyo

Alisema apozinduka alijikuta katika hospital ya Mkoa wa maweni akipatiwa matibabu baada ya kuletwa kwa msaada wa waalimu wenzie.

”Kwakweli
ni mungu tu mwenyewe ndo ameninusuru kwani nilirushwa mmara tatu na
radi na watoto wote wote darasani walikuwa wananiangukia mimi wengine
walikuwa wanakimbia ovyo nje” alisema Mwalimu Muro.