(Picha zote na Benedict Liwenga)
Na Skolastika Tweneshe
VIJANA wawili wa Shule ya Msingi International School of Tanganyika (IST) Alyanz Nasser na
Shilen Dawda wametangaza mifuko mipya ambayo imetengenezwa kwa malighafi nzuri
isiyoweza kuathiri mazingira.
Shilen Dawda wametangaza mifuko mipya ambayo imetengenezwa kwa malighafi nzuri
isiyoweza kuathiri mazingira.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwa nyakati tofauti wabunifu hao wamesema kuwa wameguswa na uharibifu wa mazingira hasa unaotokana na matumizi ya mifuko ya plastiki, hivyo wamebuni mradi wa kutengeneza mifuko ambayo haitaathiri mazingira hasa kwenye fukwe za bahari.
“Watanzania ni watumiaji wa mifuko ya plastiki hasa kwenye
fukwe hivyo maji yanapoelemewa na mifuko maji yanakuwa katika hatari.” alisema
Alyanz Nasser.
fukwe hivyo maji yanapoelemewa na mifuko maji yanakuwa katika hatari.” alisema
Alyanz Nasser.
Mbunifu mwingine Shilen Dawda ameeleza kuwa mifuko hiyo
imetengenezwa kwa ukubwa tofauti na inauzwa kati ya shilingi 400 mpaka 1200 ambapo
hadi hivi sasa wameuza jumla ya mifuko
10,000 hivyo vijana hao wanaamini kuwa kwa matumizi ya mifuko hiyo Tanzania
itakuwa safi na salama.

“Mpaka sasa tumeuza mifuko 10,000 na tunaamini kwa matumizi
ya mifuko hii Tanzania itakuwa safi na
salama na viumbe hai wataendelea kuishi.” Alisema Dawda.
ya mifuko hii Tanzania itakuwa safi na
salama na viumbe hai wataendelea kuishi.” Alisema Dawda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Rais Bwana Julius Ningu amesema kuwa Serikali
inawapongeza vijana hao kwa kuguswa na uharibifu mazingira na kuwataka
watanzania wote waunge mkono juhudi hizo za utunzaji wa Mazingira na kuacha
kutumia bidhaa zinazoharibu Mazingira.