Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula (Wa Pili Kushoto) akiwa amesimama wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe aliyeongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma, Na Balozi Job Lusinde katika zoezi la kujitolea damu kwa hiari lililofanyika siku ya leo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na Kuandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuo Hapo