BAADHI ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yosef (St. Joseph University In Tanzania-SJUIT, Dar) wameibuka katika maandamano ya kushtukiza na kwenda hadi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakiomba nao wapatiwe mgao wa fedha za Escrow kwa ajili ya kutumia kulipia ada chuoni.
Wanafunzi hao ambao walijikusanya eneo la ofisi za Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam hadi walipoondolewa na baadhi ya askari polisi walikuwa wamebeba baadhi ya mabango yaliokuwa na jumbe mbalimbali juu ya sakata la uporwaji wa kiasi cha fedha shilingi bilioni 306 ambazo zilitolewa katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Baadhi ya wanafunzi hao walisikika wakisema kuwa wanakerwa na tuhuma za baadhi ya viongozi na vigogo kujitwalia mabilioni ya fedha ilhali wao wanataseka na malipo ya ada na wengine wameshindwa kupewa mikopo ya ada na serikali kwa madai haina fedha.
Hata hivyo wanafunzi hao waliondolewa na baadhi ya askari kistarabu na kushauriwa kama wanamadai yoyote wafuate njia za kufikisha ujumbe zinazokubalika bila buguza.
Habari zaidi hapo baadaye hapahapa