|
Mgombea mwenza wa urais CCM, Bi. Samia Sukuhu (wa kwanza kulia) akipokea na kuonesha kadi anazokabidhiwa na wanachama wa upinzani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa Kimanzichana. |
|
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis (kushoto) akimvalisha nguo za sare za CCM aliyekuwa kada wa Chadema mara baada ya kuamua kujiunga na CCM. |
|
Kada wa Chadema ambaye ni kiongozi wa Vijana Kitaifa, Mtemi Nyarubanja aliyejiunga na CCM sasa akizungumza na wanaCCM na wanachama wengine. |
|
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kisarawe. |
|
Baadhi ya wagombea udiwani wa Jimbo la Mkuranga (waliokaa mstari wa mbele) wakifuatilia mkutano wa kampeni za CCM. |
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amepokea wanachama zaidi ya 460 waliotoka vyama vya upinzani CUF na Chadema na kujiunga na CCM baada ya kuvutiwa na Sera za chama hicho katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika Mkoa wa Pwani.
Mgombea huyo mwenza wa CCM, Bi. Suluhu amewapokea wanachama hao katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika maeneo anuai ya majimbo ya Mkoa wa Pwani huku akiinadi ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.
Akiwa Jimbo la Kibaha Mjini, Bi. Suluhu alipokea wanachama 47 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo pamoja na kiongozi wa chama hicho Katibu wa Hamasa Taifa wa CHADEMA, Mtemi Nyakarungu aliyeamua kukihama chama hicho pamoja na wenzake na kujiunga na CCM.
Akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM, Nyakarungu alisema amekerwa na mipango ya hujuma wanaoifanya yeye pamoja na wanachama wenzake ikiwa ni fitina za kuvidhohofisha vyama vingine na wagombea wake. Alisema baada ya kuona mambo yanaenda ndivyosivyo ndani ya chama hicho ameamua kujiengua na kujiunga na CCM ikiwa ni hatua ya kurejea kundini.
Kiongozi huyo wa Chadema alisema ataendelea kupaza sauti kuwaeleza wengine ukweli na kushawishi ili waweze kujiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na CCM chama kinachozingatia maaduli na taratibu stahiki za uendeshaji chama.
Bi. Suluhu alipokea jumla ya wanachama saba kutoka CUF waliokabidhi kadi zao katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Wilaya ya Kisarawe, huku wanachama wengine idadi kama hiyo kujiunga na CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kimanzichana na kueleza kuwa wamevutiwa na sera na ilani za Chama Cha Mapinduzi na sasa wanarudi kundili ili kuendelea kukijenga chama.
Katika mkutano wa hadhara kampeni za CCM Jimbo la Kibaha jumla ya wanachama 52 kutoka chama cha CUF walikihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, ambapo mgombea mwenza alipokea kadi zao pamoja na sare za chama hicho kabla ya kuwapa kadi mpya wanachama hao.
Akifafanua Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani alisema zaidi ya wanachama 460 wamerejesha kadi kutoka vyama vya CUF na Chadema na kujiunga na CCM katika mikutano yote ya kampeni iliyofanyika majimbo ya Mkoa wa Pwani, wakiwemo viongozi wawili wa CUF, Bi. Mwanahawa Takwanya ambaye ni Mwenyekiti wa CUF Tawi la Upendo, Umwe Kaskazini.
|
Aliyekuwa mgombea mbunge wa Mkuranga, Adam Malima akizungumza katika mkutano wa hadhara. |
|
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa hadhara Jimbo la Mkuranga. |
|
Kulia ni mmoja wa viongozi wa Chadema, Mtemi Nyarubanja akizungumza na aliyekuwa mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama. |
|
Bi. Samia Akihutubia mkutano wa kampeni wa CCM Kimanzichana. |
|
Mgombea mwenza wa CC, Bi. Samia Suluhu akihutubia mkutano wa kampeni Mkuranga. |
|
Mgombea mwenza wa urais CCM, Bi. Samia Sukuhu (wa kwanza kulia) akipokea na kuonesha kadi anazokabidhiwa na wanachama wa upinzani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa Kimanzichana. |
|
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akivunja makundi ndani ya CCM, Kati ya Adam Malima na Abdullah Ulega Jimbo la Mkuranga. |
|
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akimtambulisha mgombea ubunge wa CCM, Mkuranga Hamis Abdullah Ulega. |
|
Bi. Suluhu akipokea kadi za wanachama wapya wa CCM. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu akizungumza katika mkutano wa kampeni za CCM. |
|
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ikwiriri. |
|
Bi. Asumpta Mshama aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge akizungumza katika mkutano wa kampeni. |
|
Mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilayani Kibiti. |
|
Mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Wilayani Kibiti. |
|
Kutoka kushoto ni aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, Dk. Seif Mohamed, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Pwani Seif Mpembenue. |
|
Mgombea mwenza wa CC, Bi. Samia Suluhu akihutubia mkutano wa kampeni Mkuranga. |
|
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kampeni Ikwiriri. |
|
Adam Malima (kulia) na Dk. Seif Mohamed wakijadiliana jambo. |
|
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Seif Mpembenue akizungumza katika mkutano wa hadhara. |
|
Bi. Mwanahawa Said (kushoto) akikabidhi kadi yake ya CUF pamoja na za wenzake jumla 52 katika mkutano wa kampeni. |
|
Bi. Mwanahawa Said (kushoto) akikabidhi kadi yake ya CUF pamoja na za wenzake jumla 52 katika mkutano wa kampeni. |
|
Mwanahawa Said akizungumza na wananchi kueleza kwanini anarudi CCM na kutokea CUF. |
|
Bi. Samia Suluhu akionesha kadi alizopokea toka kwa wananchama wapyaMwanahawa Said (kushoto) akikabidhi kadi yake ya CUF pamoja na za wenzake jumla 52 katika mkutano wa kampeni. |
|
Mama Samia Suluhu akipokea baadhi ya sare ya Chama hicho. |
|
Mama Samia Suluhu akipokea baadhi ya sare ya Chama hicho mara baada ya wafuasi hao kukihama chama. |
|
Wengine wanavyotafuta njia waweze kushughudia kampeni kwa mbaaaaali. |
|
Baadhi ya wanachama toka upinzani waliorudisha fomu na kujiunga na CCM |
|
Baadhi ya wanachama toka upinzani waliorudisha fomu na kujiunga na CCM |
|
Bi. Samia akipeana mkono na wanachama wapya walioji unga na chna |
|
Msemaji wa Chama cha Mapinduzi, Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa kampeni JImbo la Kilwa Kaskazini. |