Wanachama wa Wanambwewe Waishio Dar Wakutana na Mbunge Wao

Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Mtandao wa Wanambwewe, Rajabu Papa (kushoto) akimkabidhi Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo (katikati) katiba ya umoja huo kwenye kikao cha wanachama wa mfuko huo na mbunge wao.

MBUNGE wa Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo, akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanambwewe waishio Dar es Salaam (MNDF), katika ukumbi wa Shule ya Msingi Ali Hassani Mwinyi, jijini Dar es Salaam. Wanachama hao walimwalika kwenye kikao chao cha kujadili jinsi ya kuuendesha mfuko huo kwa manufaa ya wananchi wengi

MBUNGE huyo akisisitiza jambo

Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo akizungumza wakati wa mkutano huo.

Katibu wa wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya wanamtandao wa Mbwewe waishio Dar  es Salaam, Hassani Msonde akizungumza mwanzoni mwa kikao

Mwenyekiti wa Umoja huo, Rajabu Papa akifungua kikao hicho

Mjumbe wa Kamati ya Umoja huo, Fatuma Kikwappe akisoma risala huku viongozi wakimsikiliza kwa makini akiwemo Mbunge Bwanamdogo,

Fatuma Kikwappe akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo

Mbunge Saidi Mwanamdogo akiwakabidhi dola za Marekani, viongozi wa umoja huo, ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kufanikisha usajili wa mfuko.

Mwenyekiti akimkabidi Mbunge Katiba ya Umoja

Fatuma na mjumbe mwenzake wa Kamati katika Umoja huo wakipitia makabrasha kwa makini

Mbunge wa Chalinze Saidi Mwanamdogo akiagana na viongozi wa Umoja huo baada ya kushiriki kikao. Picha kwa hisani ya Nkoromo Blog