KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na mfuko wa mafao ya uzeeni kwa watumishi wa serikalini, (GEPF) imezindua huduma itayowawezesha wanachama wa mfuko wa GEPF walioko Tanzania nzima kurejesha na kulipa michango yao ya kila mwenzi kwa kupitia huduma ya Airtel money ,
Uzinduzi wa makubaliano haya yamefanyika katika hotel ya Gold Crest
Mkoani Mwanza na kuhudhuria na Makamu wa Rais Dr Mohamed Ghalib Bilal
ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi na kushiriki kuzindua huduma hii ya pekee
itakayowawezesha wafanyakazi kulipia mafao yao bila usumbufu na kwa ufanisi
zaidi.
Katika hotuba yake Mkamu wa Rais Dr Mohamed Ghalib Bilal aliwashukuru
kampuni ya Airtel kwa kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya jamii na wateja
kwa ujumla..aidha Dr Bilal amewapongeza GEPF kwa kupiga hatua na kutafuta
njia mbadala za kuendesha shughuli zake kirahisi kwa ufanisi kwa hakika
hatua ya kutafuta changamoyo zilizopo katika ukusanyaji wa malipo, ama kwa
hakika hatua mliyoichukue niya kuigwa na vyombo vingine vya umma.
Akizungumza kwa niaba ya Airtel Meneja wa kitengo cha Airtel money Bw
Asumpya Naligingwa alisema” Airtel leo tunajisikia furaha sana kugusa
maisha ya watanzania kwa njia tofauti kupitia huduma hii ya Airtel money,
kama mnavyofahamu kwa kupitia huduma ya Airtel money wateja wetu walioko
nchi nzima wanaweza kufanya miamala mbalimbali ya fedha ikiwepo kulipa na
kupokea pesa, kulipia Luku, USA visa, kulipia Maji DAWASCO, ada za shule ,
kununua petrol kwenye vituo kadhaa nchini na nyingine nyingi, leo kwa
kushirikiana na wenzetu wa GEPF tunawezesha wafanyakazi na wanachama wote
nchi nzima kuweza kurejesha michango yao kwa kupitia huduma ya Airtel money
ambayo italeta na kuongeza ufanisi zaidi kwani sasa wateja wa Airtel
wanaweza kulipia michango hii wakiwa mahali popote, siku yoyote, wakati
wowote na bila usumbufu ”
Tunaamini kabisa ushirikiano huu utaongeza na kuendelea kutunza idadi ya
wanachama wa GEPF walioko sasa na kuleta ufanisi katika makusanyo ya
michango kwa wanachama. Wenzetu wa GEPF wataweza kuona michango mara tu
inapolipwa na pia itarahisisha njia ya malipo na kupunguza idadi ya watu
wanaoenda ofisini au bank kulipia hivyo kuokoa muda unaotumika na wanachama
kufanya malipo. Jinsi ya kufanya malipo kupitia huduam ya Airtel money ni
rahisi mteja anachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye menu ya Airtel money,
lipa bill, ingiza jina la fumbo GEPF , ingiza reference namba ambayo ni
namba ya uanachama, kisha bonyeza ndio, basi mojakwamoja akaunti ya GEPF
itapokea mchango wako na kukutumia ujumbe utakaodhibitisha malipo yako
aliongeza Naligingwa.
Naye Meneja masoko wa GEPF bwn Aloyce Ntukamazina alisema” namshukuru
makamu wa Raisi Dr Bilal kwa khudhuria halfa hii na kuwa mgeni rasmi wa
mkutano wa GEPF mwaka 2012. GEPF kwa kushirikiana na Airtel tumeanzisha
mpango utakaotupa sisi GEPF njia ya kukusanya michango ya wanachama ya kila
mwezi kwa asilimia kubwa sasa kulinganisha na hapo Awali. Tunawaomba
wanachama wetu kutumia njia hii mbadala kufanya malipo yao wakati wowote
bila usumbufu wala adha.”