Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, leo wamefunga Ofisi ya Taasisi ya Mikopo ya WADOKI (Wadoki Saccos) pamoja na Hotel ya KIRUMBA RESORT kutokana na watajwa kushindwa kulipia kodi ya pango.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid (anaeongea pichani) amesema kuwa wanachama hao wamefikia maamuzi hayo kutokana na kutumia majengo ya CCM katika kata hiyo huku wakiwa hawalipii kodi. Wanachama wa CCM katika Kata hiyo ya Kirumba wamesema kuwa, maamuzi yao yatatoa fundisho kwa wawekezaji wengine wanaotumia vitega uchumi vya Chama hicho katika maendeo mbalimbali nchini huku wakiwa hawalipii kodi ambapo wametahadharisha kwamba wale wote wenye hulka hiyo wajiandae kutumbuliwa (kuondolewa katika majengo hayo).
Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Juma Wesa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi, wamesema kuwa maamuzi yaliyochukuliwa na wanachama hayo ni sahihi kwa kuwa malalamiko ya wawekezaji hao yaliishajadiliwa hadi ngazi za juu na kuonekana kwamba wawekezaji hao hawatii makubaliano yao ikiwemo kulipa kodi ya pango kwa wakati. Meneja wa Kirumba Resort hakutaka kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba mzungumzaji ni Mkurugenzi ambae alidai amesafiri huku Uongozi wa Wadoki Saccos ukishindwa kupatikana.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid akitoa kwa wanaccm baada ya wanachama hao kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Acheni Maulidi akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Wesa Juma, akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Jane Masso ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Kirumba (kulia) amesema wanachama watahakikisha vitega uchumi vya chama vinatumika vyema kwa ajili ya maendeleo yao.
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Ulinzi wa Askari wa Kutuliza ghasia ulikuwepo ili kuhakikisha hakuna uhalibifu wowote ambao ungeweza kufanyika ambapo suala hilo limefikishwa Kituo cha Polisi Kirumba na kila upande unawasilisha vielelezo vyake ili kutambua wanaokiuka makubaliano ya mkataba wa upangaji.
Chanzo: Binagi Media Group