
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, akizungumza katika kongamano hilo.
“Ni jukumu lenu nyinyi wenyewe wanahabri muliopo ndani ya jumuia hii kuanzisha sera moja itakayo wasaidia muweze kufanya shughuli zetu katika nchi yoyoye ya jumuia bila kuzuiliwa” alisema Mwakyembe.
Dk. Mwakyemba alisema serikali haiwezi kuanzisha sera hiyo bali wenye nguvu ya kufanya jambo hilo ni wanahabari wenyewe hivyo ni vema sera hiyo ikiandaliwa waipeleke serikali ili kutengenezwa sheria itakayowapa uhuru waandishi wa jumuia hiyo kufanyakazi zao bila ya kuwekewa na kipingamizi.
bado haina nguvu katika kutetea uhuru wa mwandishi kupata habari afrika mashariki bila kuzuiwa hivyo ipo haja ya wahusika kupeleka hoja katika serikali zote ili kupatiwa mianya ya kuweka sheria itakayomlinda mwandishi kupata habari nchi yeyeote afrika mashariki bila kizuizi.
Mwakyembe ameviomba vyombo vya habari vya Afrika Mashariki kuendelea kuiboresha sekta ya habari na kuwa wabunifu ili kuweza kukuza demokrasia na maendeleo ya nchi zinazounda jumuia hiyo.
Kongamano hilo la siku moja lilihudhuriwa na wanahabari kutoka jumuia hiyo pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)