Wamachinga Wacharuka, Wavamia Ofisi za Jiji Dar

Mshike mshike wa mapambano ukiendelea muda mfupi baada ya kuwasili Jeshi la Polisi , kwa ushirikiano na mgambo wa jiji.

Mshike mshike wa mapambano ukiendelea muda mfupi baada ya kuwasili Jeshi la Polisi , kwa ushirikiano na mgambo wa jiji.

Mapambano yakiendelea kiaina kabla ya Jeshi la Polisi kuwasili eneo hilo kati ya vijana wamachinga na mgambo wa jiji.

Mapambano yakiendelea kiaina kabla ya Jeshi la Polisi kuwasili eneo hilo kati ya vijana wamachinga na mgambo wa jiji.

Eneo la barabara ya Nyerere likiwa halina msongamo kabisa baada ya watu na magari kukimbia eneo hilo kupisha mapambano ya mgambo wa Jiji na Wamachinga, waliovamia ofisi hizo.

Eneo la barabara ya Nyerere likiwa halina msongamo kabisa baada ya watu na magari kukimbia eneo hilo kupisha mapambano ya mgambo wa Jiji na Wamachinga, waliovamia ofisi hizo.

Mshike mshike wa mapambano ukiendelea muda mfupi baada ya kuwasili Jeshi la Polisi , kwa ushirikiano na mgambo wa jiji.

Mshike mshike wa mapambano ukiendelea muda mfupi baada ya kuwasili Jeshi la Polisi , kwa ushirikiano na mgambo wa jiji.

Mshike mshike wa mapambano ukiendelea muda mfupi baada ya kuwasili Jeshi la Polisi , kwa ushirikiano na mgambo wa jiji.

Mshike mshike wa mapambano ukiendelea muda mfupi baada ya kuwasili Jeshi la Polisi , kwa ushirikiano na mgambo wa jiji.

Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi vikosi mbalimbali wakiwa katika eneo la Nje ya Ofisi za Jiji mara baada ya kuwatawanya  Wamachinga.

Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi vikosi mbalimbali wakiwa katika eneo la Nje ya Ofisi za Jiji mara baada ya kuwatawanya Wamachinga.

Msafara wa magari ya magereza na washtakiwa walipita eneo la tukio hali ikiwa tete kwa kujihami kwa silaha ambapo walipita salama bila kushambuliwa. Hata hivyo walinzi wa magari hayo walionekana kuwa tayari kwa lolote baada ya kushika silaha zao mkao wa kujihami.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama eneo la makutano ya Shaurimoyo na Barabara ya Nyerere wakiangalia mapambano ya wamachinga na askari wa Jiji.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama eneo la makutano ya Shaurimoyo na Barabara ya Nyerere wakiangalia mapambano ya wamachinga na askari wa Jiji.

Hali ilivyo baada ya Jeshi la Polisi kulidhibiti eneo hilo kwa utulivu na wamachinga kutimua mbio. Pichani ni baadhi ya mgambo wa Jiji wakijadiliana mara baada ya sekeseke hilo.

Hali ilivyo baada ya Jeshi la Polisi kulidhibiti eneo hilo kwa utulivu na wamachinga kutimua mbio. Pichani ni baadhi ya mgambo wa Jiji wakijadiliana mara baada ya sekeseke hilo.

Na Mwandishi Wetu,

WAFANYABIASHARA ndogondogo maarufu kama wa machinga leo jijini Dar es Salaam waliandamana hadi katika Ofisi za Jiji la Dar es Salaam zilizopo eneo la Kamata (mataa) na kuanza kufanya fujo huku wakitupa mawe na kuchoma matairi katika barabara hiyo.

Wamachinga hao vijana ambao walikuwa wakifanya fujo hizo huku wakiimba, “..hatukubali, hatukubali, hatukubali…” waliandamana kwa kukimbia toka maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ambao baadhi yao walikamatwa na kunyang’anywa bidhaa zao na mgambo wa jiji kabla ya kufanya maandamano hayo ya kushtukiza.

Walikimbia toka Kariakoo huku baadhi yao wakiwa wamebeba mawe na vipande vya matofali ambapo walifika na kuzivamia ofisi za jiji na kuanza kurusha mawe wakipambana na mgambo ambao nao awali walikuwa wakijibishana kwa mawe na waandamaji hao. Baadhi waliwasha moto wa matairi barabarani jambo ambalo lililazimu kufungwa kwa muda Barabara ya Nyerere kupisha vurugu hizo.

Vijana hao wenye hasira waliendelea kurusha mawe katika ofisi hizo na mgambo wakijibu kwa mawe na baadaye kuanza kupiga risasi angani kuwatawanya bila mafanikio, ambapo walilazimika kukimbia ndani na kujifungia kwenye geti.

Hata hivyo vikosi mbalimbali vya Jeshi la Polisi ndio vilituliza hali hiyo baada ya kufika eneo la tukio na kuanza kupiga mabomu ya machozi na kupiga risasi hewani kuwatawanya wamachinga hao waliokuwa na jazba. Mwandishi alishuhudia polisi walio na bunduki wakipiga risasi hewani na wengine mabomu ya machozi kujaribu kuwatawanya vijana waliokuwa wakirusha mawe.

Barabara zinazopita eneo la Kamata zililazimika kufungwa kutokana na vurugu, huku shughuli zikisimama eneo hilo na baadhi ya watu kutimua mbio kujihami na vurugu zilizokuwa eneo la tukio.
Baadhi ya mashuhuda walisema vijana hao walikasirishwa na kitendo cha mgambo wa jiji kuwanyang’anya bidhaa zao na kuwatimu maeneo ya Kariakoo.

Walisema oparesheni iliyoendeshwa na mgambo hao ilisababisha mmoja wa vijana hao kujeruhiwa vibaya na gari akiwakimbia mgambo kitendo ambacho kiliwakasirika na kujikusanya kabla ya kuzivamia ofisi za jiji na kufanya fujo. Baadaye mgambo kwa hasira walianza kukamata baadhi ya waendesha pikipiki waliopita karibu na eneo lao barabarani na kuwapiga kana kwamba wanalipiza kisasi kutokana na vurugu za wamachinga.

Mtandao huu ulishuhudia mwendesha pikipiki akishambuliwa na mgambo waliokuwa hawajavaa sare nje ya jengo lililovamiwa huku wakipaza sauti wakisema; “piga, piga huyo, piga ndio hao hao…waliotuvamia.” Baadaye huku wakimpiga walimkamata na kumuingiza ndani ya jengo lao na kuikamata pikipiki yake.