Waliokufa ajali ya meli Italia wafikia watano, 17 hawaonekani

Meli iliyozama kama inavyoonekana kwa mbali majini ikiwa imezama upange mmoja.

MAITI mbili zimeopolewa tena katika meli kubwa ya kifahari ya abiria ya Costa Concordia iliyozama juzi nchini Italia eneo la Kisiwa cha Giglio. Kupatikana kwa maiti hizo kunafanya idadi ya abiria waliokuwa katika meli hiyo kufikia tano.

Mlinzi wa jirani na ajali hiyo alisema maiti za wanaume wawili wazee zimeopolewa katika upande uliozama wa meli, huku taarifa zingine zikidai bado abiria 17 hadi sasa hawajulikani walipo, sita kati yao wakiwa ni wafanyakazi wa meli na 11 abiria wa kawaida.

Waokoaji pia wamefanikiwa kumtoa mfanyakazi mmoja wa injini ya meli ambaye ameokolewa ikiwa ni saa 36 tangu kutokea kwa ajali hiyo, amekutwa amevunjika mguu mmoja. Meli ya Costa Concordia iliyokuwa na watu 4,234 yaani abiria pamoja na wafanyakazi wa meli ilipinduka usiku wa Ijumaa ya Januari 17, 2012 Ikitokea Pwani ya Magharibi mwa nchi ya Italia.

Meli ya Costa Concordia Nahodha wa meli anahojiwa, kujaribu kujua chanzo cha ajali. Aliiambia televisheni moja nchini Italia kuwa, kufuatana na ramani zake, meli ilikuwa mbali vya kutosha na ufukwe, na isingetarajiwa kugonga mwamba.

-BBC