Wakuu wa Majeshi ya Afrika Wakutana Arusha Kujadili Juu ya Tishio la Ugaidi

IMG_5429

Na; Ferdinand Shayo,Arusha.

Majenerali na Wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Barani Afrika wamekutana jijini Arusha kujadili changamoto zinazoyakibili majeshi hayo ikiwemo tishio la ugaidi ,biashara ya madawa ya kulevya suala linalopelekea majeshi hayo kuunganisha nguvu katika kupambana na matukio hayo.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa majeshi ya nchi za Afrika kwa kushirikiana na jeshi la Marekani lenye teknolijia kubwa iwapo watashirikiana na Majeshi ya Afrika kupambana na tatizo la ugaidi na kufanikiwa

Katibu Mkuu wa Wizara Ulinzi na Majeshi Job amesema kuwa jeshi la Tanzania limejipanga kukabiliana na vitendo vya ugaidi ambavyo kwa nchi ya Tanzania jukumu hilo linafanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine.

Mnadhimu wa Jeshi Marekani Jenerali Mark Milley pamoja na Balozi wa Marekani nchini Mark Childress wamesema kuwa Marekani inasubiri kupata mawazo mapya kutoka kwa majeshi ya Afrika juu ya namna ya kuimarisha uwezo na nguvu za kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Wakuu wa Majeshi ya nchi Kavu wamekutana jijini Arusha kujadili juu ya changamoto zinazoyakabili majeshi hayo ,na kubadilishana uwezo ili kuwawezesha kupiga hatua katika mapambano dhidi ya ugaidi,madawa ya kulevya,usafirishaji wa binadamu pamoja na uhalifu

IMG_5434