Wakurugenzi Bodi za Utalii Tanzania, Rwanda Wafanya Mazungumzo Berlin Ujerumani

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akiwa katika mazungumzo na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda wakati alipokutana katika maonyesho ya dunia ya Utalii ITB yanayofanyika kwenye jengo la Messe Berlin jijini Berlin Ujerumani, Monesho hayo yanahusisha makampuni yenye kutoa huduma mbalimbali za utalii duniani ambao hukutana na kutangaza utalii wa nchi zao huku wakifanya makubaliano na kuingia mikataba mbalimbali ya kuuziana bidhaa za kitalii, Maonesho hayo yanamalizika rasmi leo.

2Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani akizungumza na Ibrahim Mussa Mkurgenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii katikati ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akisikiliza kwa makini wakati Balozi huyo alipotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonesho ya ITB yanayomalizika leo jijini Berlin Ujerumani kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki.

4Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Geofrey Meena kushoto akitembelea Banda la Kampuni ya Pongo Safaris katika maonesho ya Utalii ya ITB, wengine kutoka kulia ni Marlon Van Hee Meneja Mradi wa kampuni ya ECEAT PROJECTS ya Uholanzi, Julias Alexander Pundo Mwakilishi wa kampuni ya Ramogi Tours & Travel Limited Jumuiya ya Ulaya na Cynthia Ponera Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Pongo Safaris.

6Wadau wa Ujerumani hawakukosa kutembelea maonesho hayo hapa walikuwa wakipata Menyu wakati wa hafla ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

10Team Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kazi kubwa ya kuuza utalii wa Tanzania kwenye maonesho hayo.

11Nami nikajichanganya kwenye Banda la Pongo Safaris na Ramogi Tours hapa nikipata picha na Julius wa Ramogi Tours pamoja na Cynthia wa Pongo Safaris.

12Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani wakati walipokutana katika maonesho hayo.

9

Huu nao ulikuwa ni utalii wa aina yake katika maonyesho hayo ambapo watu mbalimbali walikuwa wakipiga nao picha kwa ajili ya kumbukumbu zao. (PICHA ZOTE NA FULLSHANGWEBLOG)