Wakulima,Wafugaji na Wavuvi Kufanya Shughuli zao Kitaalam

Baadhi ya wakulima wakipata maelekezo katika PASS maonyesho ya zana za kilimo yaliyofanyika Jijini Arusha na kumalizaika jana maonesho hayo yalikuwa ya siku mbili.

Baadhi ya wakulima
wakipata maelekezo katika PASS maonyesho ya zana za kilimo
yaliyofanyika Jijini Arusha na kumalizaika jana maonesho hayo yalikuwa
ya siku mbili.

Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo (PASS) imewataka wakulima na wajasiriamali wote wa kilimo ,uvuvi na wafugaji wafikirie namna ya shughuli zao
kitaalam.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Nicomed
Bohai ya kwamba wakulima wafikirie kufanya shughuli zao
kibiashara,watafute elimu na maarifa ili waweze kudhaminiwa kupata
mkopo wa kuendeleza shughuli zao.

Amesema kuwa wanajenga mahusiano ya kibiashara kutoka kwa wafanya biashara wakubwa kwenda kwa wadogo,ili wale ambao wameshapiga hatua wawainue wale ambao bado,kwa kutengeneza mchanganuo wa kibiashara na kutoa udhamini wa mkopo.

Aidha mkurufenzi huyo amesema kuwa Asasi hiyo ya kusaidia sekta binafsi ya
kilimo ipo tayari kumsaidia mtu binafsi,vikundi au makampuni kutumia
huduma ya (Pass)haswa wajasiariamali binafsi amabao wana dira
ambao wanafanya biashara katika hali ya ufanisi na
kibiashara.

Sambamba na hayo amesema ya kwamba asasi hiyo inashirikiana na
benki washirika zaidi ya 11 kupata mkopo kwa wakulima ambao wanaoweza
kufikia angalau vigezo vya msingi kwaajili ya ukopaji,huku kipaumbele
kikitolewa kwa wateja wenye matokeo makubwa katika mwendelezo wa
mnyororo wa thamani kwa bidhaa za kilimo hususani katika mazao ya
chakula ,biashara na mazao ya kusafirishwa nje ya
nchi.

Ameainisha mikoa ambayo Pass ipo nchini Tanzania kuwa ni
Mwanza ,Kigoma,Kilimanjaro,Morogoro,Mbeya, Dar-es- salaam na
Mtwara,amesema wanatumia ofisi hizi za kanda ili kuwafikia wakulima
kwa karibu zaidi.

Nicomed Bohai Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi  ya kusaidia Sekta Binafsi
ya Kilimo Taifa  (PASS)Picha na Vero Ignatus

 

 
 
.