Wakulima Mbeya Waneemeka na Elimu ya Uzalishaji wa Mboga Mboga kutoka TAHA

Codes

 Dr. Christine Ishengoma Mkuu wa Mkoa wa Iringa akipokea taarifa kuhusu mfumo wa taarifa za masoko kutoka TAHA unavyofanya kazi zake kutoka kwa Cyrila Antony Afisa wa Masoko
Mkuu wa mkoa wa Iringa  Mh. Dr. Christine Ishengoma akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa kilimo wa TAHA Bw Ringo kuhusu uzalishaji wa zao la nyanya 
Elimu ikiendelea kutolewa

 Vitalu na green houses

 Aina Mbalimbali za matunda ambazo zimezalishwa na wakulima kutokana na elimu Bora waliyo ipata kutoka TAHA

 Mwananchi akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa TAHA

 Teknolojia ya umwagiliaji kwa mfumo wa kilimo cha matone ambao pia unaonesha utengenezaji bora wa matuta, nafasi na usafi

Hivi ni  Vitalu vya TAHA na Barton Tanzania

 Vitalu vya mboga na green house kama zinavyoonekana katika picha

 Watangazaji wa Radio Sweet FM ya Mbeya wakishangaa ubora wa karoti ambayo ni daraja la kwanza inapopelekwa sokoni

 Zao la chines

Zao la karoti lililopandwa kwenye vitalu vilivyopo ndani ya viwanja vya Nanenane Mbeya kwenye Banda la TAHA

 Mwananchi akifurahia maelezo kuhusu zao la karoti daraja la kwanza



********************

Wakulima na wananchi mkoani Mbeya
wameendelea kuneemeka na elimu ya bure ya uzalishaji wa mazao ya mboga, viungo
na matunda inayotolewa na Asasi ya wakulima, wafanyabiashara na watoa huduma ya
mazao ya horticulture nchini Tanzania (TAHA).
 
Wakulima hao wameneemeka na elimu
hiyo inayotolewa na maafisa wa ufundi wa kilimo kutoka TAHA kwa ushirikiano na
wale wa Barton Tanzania ambao kwa pamoja wameweka kambi katika viwanja hivyo
ili kuhakikisha jamii ya wakulima wa mboga kutoka ukanda wa Nyanda za Juu
Kusini wanapata elimu ya msingi bora ya uzalishaji wa mboga wenye tija.
 
“Mpaka sasa tumetembelewa na
wananchi na wakulima wasiopungua 460 ambao wamefika katika banda letu hapa
Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale wakitaka kujifunza mbinu na misingi
ya awali ya uzalishaji wa mazao ya horticulture, hiyo ni ishara njema kwani
inaonesha ni kiasi gani wananchi
wanatafuta mbinu fasaha inayoweza kuwakwamua kutoka katika uzalishaji wa
mboga wa kawaida mpaka uzalishaji wa tija unaozingatia viwango vya kitaifa na
kimataifa” Alisema Likati Thomas afisa Mawasiliano kutoka TAHA.
Akifafanua zaidi kuhusu elimu ya
kilimo cha uzalishaji wa mboga kwenye banda la TAHA afisa mawasiliano huyo
alisema kuwa wamepanda mazao tofauti katika ploti zilizopo kwenye eneo lao
ambapo wakulima na wananchi wanaopata fursa ya kutembelea eneo hilo ujifunza
teknolojia mbalimbali za uzalishaji kama vile uzalishaji unaozingatia Mbegu
bora zenye tija.
 
Teknolojia nyingine ni pamoja na
upandaji mazao unaozingatia nafasi kati ya miche na miche, umwagiliaji kwa njia
ya matone(drip irrigation) unaozingatia uhifadhi wa maji na mazingira pamoja na
ulimaji wa matuta yaliyoinuka ili kutoa nafasi kwa mizizi ya mimea kupenyeza
kwenye udongo ili kujitafutia lishe.
 
Mbali na elimu hiyo ya uzalishaji
wa mboga, wananchi wa Mbeya wanaotembelea banda hilo pia wanapata fursa ya
kujifunza elimulishe kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi.
Lawrencia …..ambaye amekuwa akiwafundisha wananchi juu ya umuhimu wa ulaji wa
mboga na faida zake kwa afya ya miili yetu.

 

Kawaida