Wakazi wa Jangwani Waanza Kurejea Kwenye Makazi Yao Licha ya Maafa Yaliyowakuta!

20140424-204612.jpg

20140424-204633.jpg

20140424-204645.jpg

Kama picha zilivyonaswa na thehabari hapo juu, inaonekana wakazi wa Jangwani wakirejesha makazi yao licha ya maafa makubwa yaliyowakuta kutokana na mvua kubwa zilizolikumba jiji la Dar hivi karibuni. Magodoro na vifaa mbalimbali vilionekana vikiwa vimeanikwa juu ya mapaa na kwingineko, tayari kuanza maisha mapya.

Inasemekana serikali iliwahamishia wakazi hao eneo la Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni, lakini inaonekana baadhi yao bado wameanza kurudi hapo Jangwani. Pamoja na hayo, thehabari imedokezwa kwamba serikali ilitumia mamilioni ya shillingi kuboresha miundombinu eneo hilo.

Picha zote na Mpiga Picha Maalum wa Thehabari, Dar-es Salaam.