Wananchi na wakazi wa maeneo ya Tabata Liwiti wakiwa katika foleni ya kupiga kura leo jijini Dar es Salaam.
|
Wananchi na wakazi wa Tabata Shule wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura yao. |
|
Wananchi na wakazi wa maeneo ya Tabata Liwiti wakiwa katika foleni ya kupiga kura leo jijini Dar es Salaam. |
|
Mkazi wa eneo la Matumbi akipiga kura yake leo. |
|
Mkazi wa Kawe akipiga kura yake leo. |
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo wamesimamisha shughuli zao na kushiriki zoezi la upigaji kura kuchangua viongozi wanaoona wanafaa kwa ajili ya kuwaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Viongozi waliokuwa wakipigiwa kura leo ni wa ngazi ya udiwani, wabunge na nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zoezi katika maeneo mengi ambayo mtandao huu ulitembelea ya Tabata, Ubungo, Sinza, Magomeni, Kigogo, Buguruni, Matumbi, Mwananyamala, Kawe pamoja na Kijitonyama zoezi limeenda vizuri huku idadi kubwa ya wapiga kura wakijitokeza kutimiza haki yao ya msingi. Maeneo mengi vijana wameonekana kujitokeza kwa kiasi kikubwa huku vituo vingi vikitawaliwa na amani na utulivu katika vituo hivyo. Licha ya changamoto ndogondogo ambazo zilikuwa zikijitokeza kama baadhi ya wakazi kukosa majina yao kwenye orodha waliweza kupewa mwongozo ya nini cha kufanya na wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi. Ramadhan Mabula ni Msimamizi wa Kituo Kata ya Ubungo akizungumzia eneo hilo alisema zoezi kwa kiasi kikubwa linaendelea vizuri na zipo changamoto ndogondogo ya baadhi ya watu kutoona majina yao lakini utatuzi umetolewa na ofisi za juu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wanaendelea na zoezi vizuri. Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa vituo vya Kata ya Kigogo, Daudi Chambo alisema vituo vyote 59 vilivyopo sehemu mbalimbali katika Kata hiyo zoezi linakwenda vizuri na hata wananchi waliokuwa wakijitokeza kulalamika kutoona majina yao walisaidiwa na baadaye kupiga kura. “…Unajua wapo waliokuwa wakilalamika hawaoni majina yao lakini ukifuatilia kiundani unakuta alikuwa akitafuta jina sehemu ambayo sio na aliposaidiwa aliweza kupiga kura na kuondoka,” alisema Chambo. Licha ya idadikubwa ya wananchi kufika vituoni mapema zaidi yaani saa kumi za asubuhi na saa kumi na mbili zoezi limeanza majira ya saa moja asubuhi na wapiga kura kuendelea na upigaji kura huku wakiongozwa na wasimamizi na makalani vituoni. Katika vituo ambavyo vimetembelewa hakuna vilivyokwama kutekeleza shughuli hiyo ya upigaji kura.
|
Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wa ndani ya nchi wakijadiliana jambo wakiwa kazini katika kituo cha Tabata Liwiti. |
|
Maeneo mengine foleni zilitembea haraka kiasi cha kumalizika mapema… |
|
Eneo la Ubungo ambalo muda wote huwa na idadi kubwa ya watu na mishemishe nyingi leo lilikuwa shwari… |
|
Foleni za wapiga kura eneo la Ubungo… |
|
Baadhi ya waangalizi wa kimataifa wakifuatilia zoezi la upigaji kura kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam.. |
|
Foleni ya wapigakura Kata ya Ubungo.. |
Maeneo mengi ya jiji hata yale ambayo huwa yamechangamka leo yalikuwa yamesimamisha shughuli zake na watu kuelekea kutimiza wajibu na haki yao ya msingi ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowapenda. Mwandishi wa habari hizi ametembelea maeneo ya Ubungo, Sinza, Msasani, Kawe, Magomeni, Kinondoni na mengineyo ambapo idadi kubwa ya maduka yalikuwa yamefungwa na hakuna mikusanyiko ya watu hali inayoonesha wamesimamisha shughuli kutekeleza zoezi la kupiga kura. Tayari vituo vingi vimehitimisha zoezi la upigaji kura na kujipanga kuanza kujumlisha kura kabla ya kutoa matokeo kama taratibu zinavyoelekeza. Endelea kuwa nasi tutakuletea matokeo kituo baada ya kituo kadri tunavyo yapokea.
|
Maeneo mengine makarani na wasimamizi waliwasubiri wapiga kura… |
|
Foleni ya wapiga kura Mwananyamala Jijini Dar es Salaam… |
|
Maeneo ambayo muda wote huwa bize leo hali ilikuwa ni tofauti, yaani yalikuwa kimyaaa kupisha zoezi la upigaji kura… |
|
Wapiga kura na wakazi wa Kawe wakiendelea na zoezi hilo bila tatizo lolote… |
|
Wananchi Kata ya Magomeni wakitimiza wajibu wao wa kuchagua viongozi… |
|
Zoezi likimalizika eneo la Kituo cha Kigogo jijini Dar es Salaam… |