Wajua kuwa sasa unaweza kujipima UKIMWI nyumbani kwako?

Hii ni furaha kwa kila mmoja, wajua kwamba sasa unaweza kujipima Ukimwi nyumbani?

MAREKANI imetangaza kuruhusu kuuzwa kwa chombo cha kupima virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa binadamu vya HIV. Baada ya kifaa hicho maalumu cha vipimo kukubalika na kuruhusiwa mtu anaweza kujipima UKIMWI mwenyewe akiwa nyumbani. Chombo hicho ambacho sawa na kijisanduku kidogo kitamsaidia mtu kujipima wenyewe virusi vya HIV nyumbani bila msaada wa mtaalamu wa afya.

Badala ya utaratibu wa sasa wa kwenda hospitalini na katika vituo maalumu vya Afya kutambua afya yake. Kiongozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa wa taifa hilo (FDA) na Kampuni iliyofanikisha kutengeza kikasha hicho ‘OraSure Technologies’ cha kupima virusi vya HIV1 na HIV2, kwa pamoja wanasema hatua za tekinolojia hiyo ni kubwa katika kupambana na maambukizi ya UKIMWI.

Wamesema anachotakiwa mtu kufanya ni kuchukuwa ute au mate yaliyopo katika kinywa chake kwa kutumia vifaa maalumu na kusugua katika fizi za juu na chini kisha kuweka ute huo katika kipimo ambapo baada ya dakika kati 20 na 40 jawabu hupatikana

Kifaa hicho kinatarajiwa kupatikana kwa matumizi mwezi Oktoba mwaka huu kwa wauzaji wa maduka ya rejareja zaidi ya 30,000 watakaokuwa na uwezo wa kuuza kifaa hicho ambacho kinaweza kuwa msaada wa kupunguza safari za watu kwenda vituo vya afya kupima.

Mamlaka ya Chakula na Madawa ya Taifa hilo imesema ni kweli kifaa hicho kinauwezo wa kupima ukimwi lakini katika watu 12 watakaopima mtu mmoja kuna dalili ya kuwa na majibu chanya wakati hana virusi vya ugonjwa huo ambao ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vya watu wengi duniani.

Lakini ufanisi wake ni kwa asilimia 92 wakati asilimia 8 inayobakia ndipo anaweza kupatikana mtu mmoja kuwa na majibu chanya wakati majibu yake ni hasi. Huwezo wa kifaa hicho unawekwa wazi kuwa unaweza kutambua aina mbili za virusi vya UKIMWI yaani HIV namba 1na HIV namba 2 ambavyo hapo awali ilikuwa vigumu kuweza kutambua kwa kipimo kimoja.

Hali ya kwenda kwa wataalamu wa Afya kupata uhakika wa kupima haiepukiki kwani katika kila anayepima anashauriwa kuwaona wataalamu hao kuhakikisha suala hilo kwani si uhakikia wa asilimia100.

Kulingana na utafiti mwingine uliofanya juu ya huwezo wa kipimo hicho unasema wazi kuwa kati watu 5000 wanaopima ni mtu mmoja tu anatapa majibu yasiyo sahihi kwa ungowa huo, ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Taifa hilo wanasema wanakubaliana nalo.

Naye Msemaji wa Kampuni hiyo ya OraSure Technologies anasema bei ya kifaa hicho ni sawa na Euro 17 ambayo sawa na shilingi 3400 za Kenya na sawa na sh. 34,000 za Tanzania.

Wakati huo huo Rais na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Douglas Michels anasema kifaa chao kitawasadia mno watu kupima na kutambua hali ya maambukizi ya UKIMWi kwa amani wakiwa nyumbani na wataklwenda kuwaona madaktari pale watakapo takiwa kufanya hivyo kwa matibabu zaidi.

Kulingana na kituo cha Kupambana na Kujikinga na Mangojwa cha Marekani mpaka sasa nchi hiyo ina watu milioni1.2 wanaoishi na virusi vya HIV ambapo katika kila Wamerekani watano mmoja hatambui uzima wahali yake ya afya kama ana virusi hivi au la, huku kila mwaka watu 50,000 wanaambukizwa virusi vinayosababisha UKIMWI.