Wajasiliamali Watakiwa Kuwa na Mipango Madhubuti

22222

WANAWAKE Wajasiriamali nchini wametakiwa kuwa na mshikamano, uthubutu, na upendo ili kusonga mbele katika shughuli zao za kiuchumi.

Mwito huo ulitolewa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya Tanzania (NFNV), Emma Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga mkutano wa kupanga na kuweka mikakati ya vikundi vya umoja na umoja wa kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa mwaka 2017

Mkitaka kusonga mbele kiuchumi kupitia ujasiriamali wenu kama wanavyo fanya wanawake wenzetu katika nchi mbalimbali duniani mnapaswa kuwa na uthubutu, kupendana, kuacha majungu, kutunza muda  na kushirikiana” alisema Kawawa

Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa alisema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha viongozi wa vikundi vya umoja wa wanawake kwenye masoko ya Manispaa  ya Ilala na Temeke ili kuweza kujadili changamoto za uendeshaji na uimarishaji wa umoja masokoni kwa mwaka 2017

Malengo mengine ya mkutano huu ni kutengeneza mpango kazi wa kufufua na kuimarisha umoja masokoni kwa mwaka 2017, kupeana mrejesho wa usajili wa umoja wa kitaifa (Uwawasota) na kupokea taarifa ya kamati ya uhamasishaji wa umoja kwa mwaka 2016″ alisema Mlawa

Ofisa Uwezeshaji Jamii Kiuchumi wa Shirika hilo, Theresia Jeremia alisema mkutano huo uliwahusisha wanawake wajasiriamali kutoka masoko sita ya katika manispaa za Temeke na Ilala ambayo ni Gezaulole, Tabata Muslimu, Ferry, Temeke Sterio na Mchikichini