Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene ametembelea eneo la viwanda vidogo, SIDO na kuwataka wajasiliamali kuamka na kuacha kuwa wategemezi kwa kila jambo huku wakinyooshea kidole Serikali juu ya changamoto zinazowakabili.
Waziri Mbene ametoa changamoto hiyo jana jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa umefika wakati wa viwanda vidogo kuendesha uchumi wa nchi kwa kujipanua katika kila nyanja na kuacha kujichimbia sehemu moja na kuacha masoko yakishikwa na wageni.
“Tatizo lililopo ni wengi wenu bado mna mawazo ya mashirika ya umma kwa kuwa mpo chini ya shirika la umma hivyo kama mkiendelea hivyo amtakuwa bali mtadumaa katika kazi zenu za kila siku ni vyema mkafungua milango na kutafuta wadau mbalimbali ambao mnaweza kufanya nao biashara za bidhaa mnazo zalisha,” alisema Waziri Mbene.
Aliongeza kuwa ni vyema wakatumia fursa ya kukutana na wabunge hili waweze kuwaeleza ni namna gani mashine zao na bidhaa wanazozalisha zitakavyoweza kupunguza umaskini kwa makundi ya vijana yaliyopo katika majimbo yao na kuondoa dhana ya malalamiko ya viajana kuwa nchi hii aina ajira na matokeo yake kujiajiri wenyewe.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanaga ambaye aliambatana na Naibu waziri Mbene katika ziara hiyo alisema kuwa wizara yake inalichukulia swala la uwepo wa viwanda vidogo kama sehemju ya kufikia malengo ya nchi kwa kutoa ajira kwa kila mtanzania kwa namna moja hama nyingine.
Alisema kwa wastani kiwanda kidogo kinaweza kutoqa ajira ya watu nane kwa kila kimoja hivyo kama kwa kila kata kukiwa na viwanda vinne tu ajira zitakuwa nyingi san kuliko tunavyofikiri hivi sasa kutegemea kuajiriwa na serikali kuu peke yake.