Watu watatu wakazi wa wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro wamehukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mauaji
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama kuu kanda ya Moshi iliyokuwa ikiendesha vikao vyake katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo chini ya Jaji Amaisario Munisi
Awali kabla ya kusoma kwa hukumu hiyo mwanasheria wa Serikali Tamari Mndeme aliwataja watuhumiwa wote watatu kuwa ni Plasid Herman, Wiliadi Evaristi na Samsoni Kanje Myovela wanaokabiliwa na tuhuma za kumuua kwa maksudi mkazi wa Kijiji cha Nayeme tarafa ya Tarakea,Anastazia Nicodemu
Alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Mei 23, 2010 katika kijiji cha cha Nayeme Tarfa ya Tarakea wilayani Rombo,mkoani Kilimanjaro
Mndeme amedai mahakamani hapo kuwa kesi inayowakabili watuhumiwa hao walilitenda Mei 23 2010 kwa kumuua kwa makusudi anastazia Nicodemu kinyume na kifungu cha 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Munisi ambaye alianza majira ya saa 14:21 mchana na kukamilisha saa 15:26 ameisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka na utetezi haubishaniwi kuhusu kifo cha marehemu.
Alisema katika kutetea hoja zao upande wa mashtaka ulileta mashahidi 6 ambao wote kwa pamoja wakiongozwa na shahidi namba moja waliwatuhumu washtakiwa kuhusika na tukio hilo.
Alinukuu kielelezo namba Moja kilichowasilishwa na hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo Usseri ambaye alimwandikia maelezo ya ungamo ambapo Mshtakiwa namba tatu alikiri kuwa yeye na wenzake wawili walienda nyumbani kwa marehemu majira ya saa tatu usiku kwa ajili ya kwenda kumdaifedha yao kiasi cha tsh 9600 ikiwa ni malipo yao ya kupukuchua mahindi lakini walipofika walimkosa nyumbani na hivyo wakapanda ukuta wa nyumba yao na kuingia ndani ambapo walijificha uvunguni mwa kitanda chake na aliporudi walimshambulia kwa mapanga na ksabababishia kifo chake.
Kutokana na ushahidi huo alisema Mshtakiwa namba moja na namba mbili wanatiwa hatiani kuhusika moja kwa moja na mauaji kutokana na ukiri wao kwa mlinzi wa amani, Mchukua maelezo na shahidi namba tatu ambaye ni mume wa marehemu ambaye anadai kuwa alishuhudia wakitekeleza tukio hilo na kuwatambua wahusika
Kutokana na utetezi huo, Jaji munisi alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuthibitisha kuhusika pasipo shaka kwa washtakiwa wote watatu kwa mujibu wa sheria kifungu cha 197 ya sheria ya kanuni ya adhabu washtakiwa hao adhabu yao ni kunyongwa hadi kufa