Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Leph Gembe akiingia Ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) aliyemaliza muda wake Bw Emmanuel Misungwi katika ukumbi wa veta uliopo Mkoani Dodoma katika Sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu Mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini (Wa Pili Kushoto)Mh Leph Gembe akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao wamemaliza muda wao ambapo wa kwanza kushoto ni Mwalimu mlezi wa taasisi hiyo Bw. Jeremiah katika sherehe ya Kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia
Wawakilishi wa wanafunzi walioitwa mbele kwaajili ya kukata keki kutoka kushoto ni Mwanafunzi Loyce Haule, Katikati ni Shabani Kambi na Mwisho kabisa Ni Beatrice Msami