UMOJA wa Mataifa (UN) umebainisha kuwa wahamiaji wapatao 700 wanahofiwa kufariki katika kipindi cha siku tatu zilizopita katika bahari ya Mediterranean.
Msemaji wa Shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi (UNHCR), Carlotta Sami, amesema mashua kadhaa zimezama katika maeneo ya kusini mwa Italia Jumatano usiku ikiwa na wahamiaji hao.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya wahamiaji waliookolewa zinaeleza kuwa juma lililopita walishuhudia boti moja kwenye bahari ya Mediterania ikizama ikiwa pamoja na wakimbizi waliokuwa wakiitumia kusafiria.
Shirika moja la uokoaji la Save the Children, limeiambia BBC kuwa manusura hao walisema kuwa waliondoka katika msafara wa maboti matatu Jumatano usiku kutokea Libya.
Maafisa wa Polisi wa Italia wanasema waliwahoji wahamiaji hao waliofika mjini Sicily hapo Jumamosi. Juma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterania.
-BBC