Bango la hospitali ya Temeke, linalo onyesha utaratibu wa kuona wagonjwa kama lilivyonaswa na Mpiga picha wetu.
Ndugu ambaye hakufahamika jina lake, akiongea na mgonjwa wake, ambaye amelazimika kulala chini ndani ya wodi namba 4 kwenye hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Temeke. Uchunguzi wetu uligundua kwamba, hospitali hizi zimepandishwa hadhi mwaka jana na kuwa hospitali za rufaa za mkoa. Cha kusikitisha ni dhahiri kwamba hadhi ya huduma bado haijapandishwa.
Mpiga picha alishuhudia baadhi ya wagonjwa wakiwa wamelazwa wawili wawili. Ndugu wa wagonjwa wanazuiwa kulala na wagonjwa wao, lakini hali za wagonjwa hospitalini zinaonyesha dhahiri kuwa watoa huduma wamezidiwa! Mpiga picha wetu alishuhudia mgonjwa mmoja akiwa amejichafua vibaya na matapishi huku kukiwa hamna dalili za msaada. Hali ambayo ni tishio kwa afya za wagonjwa wengine na wageni waliokwenda kutembelea wagonjwa wao.
Wagonjwa
Nesi akiwa anaelekea kwenye moja ya wodi hospitalini hapo.
Nesi.
Picha zote na Mpiga Picha Maalum wa thehabari, Dar.