SERIKALI nchini Canada imesema kuwa itatoa hadi dosi 1,000 za chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola kwa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO. Hali hiyo imefikiwa ikiwa ni kusadia kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika ambao hadi sasa umewaua zaidi ya watu 1,000.
Taarifa za kiafya zinasema hatua hiyo pia imefikiwa baada ya shirika la afya duniani kusema ni sawa kimaadili kutumia dawa ambayo bado haijafanyiwa majaribio kutibu wagonjwa katika hali ya dharura.
Waziri wa afya nchini Canada, Rona Ambrose alisema kuwa nchi hiyo imetengeneza karibu dosi 500 za dawa hiyo lakini haijafanyiwa majaribio kwa binadamu. Wataalamu wanaonya kuwa huenda ikachukua hadi miezi sita kutengeneza kiwango cha dawa ambacha kinaweza kutumiwa.
Kampuni moja ya kimarekani ambayo ilikuwa imetengeneza dawa za majaribio ilisema kuwa kwa sasa kiwango cha dawa ilicho nacho ni kidogo kulingana na mahitaji.
-BBC