Wagonjwa wa Akili Watoroka Hospitalini Kenya, Boko Haram wamewateka Watoto

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

POLISI wanawatafuta wagonjwa karibia arobaini waliotoroka kutoka hospitali ya watu wenye matatizo ya kiakili, mjini Nairobi ya Mathare. Wagonjwa hao wanasemekana waliwashinda nguvu walinzi wao na kutoroka.

Zogo hilo lilizuka katika hospitali ya Mathare baada ya kutokea hali ya sintofahamu iliyowahusisha wafungwa arobaini wanaume. Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa wagonjwa hao walikuwa wanateta kuhusu hali mbaya na kibinadamu katika hospitali hiyo.

Wakati huo huo, wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake na watoto katika kujibu hatua ya jeshi kuwakamata wake za wanachama wa kundi hilo pamoja na watoto wao. Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alitoa kanda ya video inayoonyesha wanawake na watoto waliowakamata.

Habari zinazohusianaMakao ya polisi yashambuliwa NigeriaKiongozi wa Boko Haram akombolewaTaarifa zinazohusianaSiasaIkiwa hili litathibitishwa, watakuwa mateka wa kwanza raia wa Nigeria kutekwa nyara na kundi la Boko Haram. Shekau pia alisema kuwa kundi hilo ndilo lilifanya mashambulizi mawili ya hivi karibuni Kaskazini Mashariki mwa nchi ambayo yaliwaacha takriban watu 240 wakiwa wameuawa.

Kundi hilo limekataa msamaha uliotolewa kwao na serikali ili waweze kuacha vurugu zao ambazo zimesababisha vifo vya watu 2000 katika miaka mitatu iliyopita. Kundi la Boko Haram, limekuwa likituhumu vikosi vya usalama kwa kuwazuia kinyume na sheria jamaa za wapiganaji wa Boko Haram likisema kuwa kuachiliwa kwao itakuwa kikwazo cha kuwa na mwafaka wowote.

Kwenye kanda hiyo, Shekau hakusemna chochote kuhusu idadi ya wanawake na watoto waliokamatwa.
“tuliwakamata wanawake na watoto kadhaa pamoja na vijana barobaro,” alisema bwana Shekau.
-BBC