Na Janeth Mushi, Arusha
WAKAZI 33,422 wa jamii ya wafugaji wanaokabiliwa na tatizo la njaa wilayani Longido mkoani hapa wamenufaika na mradi toka Shirika lisilo la kiserikali la World Vision wa kutoa huduma ya msaada wa chakula kwa wananchi wanaokabilwia na tatizo hilo.
SHIRIKA la World Vision Tanzania limezindua mradi wa kutoa huduma ya
msaada wa chakula cha lishe kwa kugawa tani 802 zenye thamani bilioni
1.2 kwa wakazi 33,422 wa jamii ya wafugaji wanaokabiliwa na tatizo la
njaa.
Akizungumza katika Uzinduzi wa mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa World Vision Tanzania, Tim Andrews juzi, alisema kuwa mpango huo unatekelezwa katika mikoa iliyoathiriwa na tatizo la ukame ambayo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tabora, Singida na Shinyanga.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kutokana na mikoa hiyo kukubwa na ukame wakazi wake wengi wamekabiliwa na njaa huku walengwa katika mpango huo wakiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano, akina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha.
“Kupitia mradhi huu katika wilaya hii ya Longido tutahudumia watu zaidi ya 4,319 ambao hawana uwezo wa kujinunulia chakula na wanakabiliwa na njaa na katika kundi hili watoto walio katika umri wa chini ya miaka mitano ni 1,330,” alisema Tim.
Aidha takwimu katika wilaya hiyo itakayopata tani 158 kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi septemba hadi Novemba, akina mama ambao wanaonyonyesha ambao watanufaika ni 1,484 huku akina mama walio wajawazito ambao irodha yao imepatikana kupitia mahudhurio yao ya kliniki ni 577.
Katika uzinduzi wa mradi huo tani za unga wenye virutubisho ziligawanywa kwa walengwa ambapo kila mmoja wao alipata kilo sita (6) na mgao huo watakuwa wakiupata wka kiasi hicho cha kilo sita kwa kila baada ya wiki mbili.
Naye Meneja Miradi wa shirika hilo, Devoctus Kamara alisema katika kipindi hicho cha Septemba hadi Novemba maeneo yanayokabiliwa na njaa katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha itapata tani 380 cha unga wenye virutubisho.
Kamara alisema kuwa katika mkoa ya Kanda ya Kaskazini watu zaidi ya 15,823 watagawiwa unga huo wa liseh ambao thamani yake ni Dola za Kimarekani 380,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 570 za Kitanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Longido James Ole Millya aliwataka wakazi haow ajamii ya kifugaji kuzingatia mila na desturi zao zilizokuwa zinatumika kuwatunza akina maama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka mitano kwa kuwapa maziwa kama lishe, badala ya kuuza maziwa yote wanayoyapata kwa ajili ya kujipatia fedha.
Ole Millya alitumia fursa hiyo kwa kuisihi jamii hiyo ya kimasai kuwa na mabadiliko, kwa kuacha kufuga mifugo kama mazoea na badala yake kufuga kwa kutumia mbinu za kitaalam wanazoelekezwa na wataalamu ili waweze kunufaika na mifugo yao.