Na Joachim Mushi
JUMLA ya wafanyakazi 32 kutoka makampuni, taasisi na idara mbalimbali nchi wamepewa dhawadi ya vyeti pamoja na fedha viwango tofauti baada ya kuibuka wafanyakazi bora na hodari kitaifa katika kampuni na taasisi wanazofanyia kazi. Majina ya wafanyakazi hao yalitajwa jana jijini Dar es Salaam pamoja na kukabidhiwa zawadi zao kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru na kuongozwa na Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Walioibuka wafanyakazi bora na kukabidhiwa vyeti pamoja na fedha ni pamoja na Bw. Nkonze Masuha kutoka chama cha TEWUTA ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) aliyejipatia kitita cha shilingi 1,000,000 na Bw. Herman Kachima kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF, Makao Makuu jijini Dar es Salaam aliyezawadiwa kiasi cha shilingi 5,000,000.
Wafanyakazi wengine walioibuka wafanyakazi bora (kwenye mabano kiasi cha fedha walichozawadiwa) ni pamoja na Sifuni Fadhili wa Bodi ya Korosho Tanzania (2,000,000), Robert Banda wa Alliance One TOBACCO LTD (1,000,000), Dominic Malela wa Kilombero Suger Co. LTD (1,500,000), Peter Gawile wa TPA Makao Makuu (1,200,000), Danstun Rima wa TPA Makao Makuu (1,200,000), Joseph Kibonge wa Tanesco Loliondo (TV thamani ya 2,200,000 na fedha 3,000,000), na Catherine Kilinda wa AICC Arusha (3,600,000).
Wengine ni pamoja na Felix Mushi wa Wazo Hill Cement (2,500,000), Simon Shimbi wa NHC (2,000,000), Chrispianus Bahaako wa TANROADS (1,500,000), Hamis Mdoe wa STAMICO (1,500,000), Lecian Mgeta wa TEMESA Makao Makuu (2,000,000), Bertha Sule wa Haydom Rutheran Hospital (1,000,000) na Lodovick Utouh Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali .
Wengine ni pamoja na Juliana Genda wa Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro(3,000,000), Eunice Urio wa VETA (5,000,000), Henry Pambila wa VETA (3,000,000), Gaudence Temu wa SwissPort (T) Ltd (6,000.000) , Sera Mgome wa SwissPort (T) Ltd (3,000,000), na mfanyakazi Joseph Kekokere wa Shirika la Posta (1,500,000), pia wengine ni walimu saba kutoka Chama cha Walimu Tanzania na wengineo.