Wafanyabiashara Dar wanufaika na mafunzo ya kijasiliamali

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana akizungumza kufungua mkutano wa wafanyabiashara wa Dar es Salaam “NMB Business Club’ waliokutanishwa na benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.

 

Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa ‘”NMB Business Club’ waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.

 

Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa “NMB Business Club’ waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Takribani wafanyabiashara zaidi ya 500 walishiriki mkutano huo wa mafunzo ya biashara jijini Dar es Salaam.

 

Mwenyekiti wa NMB Business Club Mkoa wa Dar es Salaam, Ezekiel Gutti akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa ‘”NMB Business Club’ waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Takribani wafanyabiashara zaidi ya 500 walishiriki mkutano huo wa mafunzo ya biashara jijini Dar es Salaam.

 

Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo.

 

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa Dar es Salaam “NMB Business Club’ waliokutanishwa na benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.

 

Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa ‘”NMB Business Club’ waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.

 

Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za mikopo na ukuaji wa biashara zao.

BENKI ya NMB imekutanisha wafanyabiashara zaidi ya 500 wa jijini Dar es Salaam waliopo katika jumuia ya wafanyabiashara wa NMB “NMB Business Club” kwa lengo la kutoa mafunzo mbalimbali ya biashara pamoja na mafunzo ya kodi ili kukuza biashara zao.

Kundi hilo la NMB Business Club mkoa wa Dar es Salaam limekutanishwa kwa pamoja ili wafanyabiashara hao waweze kujuana na kubadilishana uzoefu katika shughuli zao jambo ambalo litachangia wao kushikamana na kunufaika zaidi na huduma zinazotolewa na benki hiyo.

Akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano huo, Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela alisema katika semina hiyo wataalam wa biashara wa Benki ya NMB watatoa mafunzo mbalimbali ya namna ya kukuza biashara na kuelezea fursa anuai zilizopo ndani ya benki hiyo ili wateja wao waendelee kunufaika nazo.

Alisema mbali ya kutoa mafunzo ya biashara na kodi wana NMB Business Club walioshiriki katika mkutano huo watapata fursa ya kutoa mrejesho dhidi ya huduma wanazopewa ili benki iangalie namna ya kuzishughulikia.

Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo.

 

Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za mikopo na ukuaji wa biashara zao.

 

Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za mikopo na ukuaji wa biashara zao.

 

Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo.

Awali mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana akifungua mkutano huo aliwataka wafanyabiashara hao kutambua kuwa Serikali inawategemea wafanyabiashara katika kukuza jiji kupitia huduma mbalimbali za kibiashara ambzo wanazitoa kwa jamii.

Alisema Serikali kupitia ofisi yake itaendelea kujenga mazingira bora ya wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa maendeleo na kuwaomba walipe kodi kama inavyotakiwa kwenye biashara zao, kwani hii ndio njia pekee ya kuboresha huduma na maendeleo kwa jamii.

“…Mtambue ya kwamba katika huduma mnazozitoa kibiashara mbali ya kunufaika nyinyi mnachangia kuleta maendeleo, pia mnapendezesha jiji letu…inapaswa mtambue ni watu muhimu sana katika kujenga uchumi,” alisema Mkurugenzi huyo wa jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa NMB Business Club Mkoa wa Dar es Salaam, Ezekiel Gutti alisema wafanyabiashara walioalikwa katika mkutano huo ni ambao wamekuwa wakinufaika na huduma mbalimbali za mikopo na ushauri wa kifedha kutoka kwa benki ya NMB na wanafanya vizuri katika biashara zao na hata marejesho kwa mikopo mbalimbali wanayoomba benki.