Wafanyabiashara 2000 Kunufaika na Njia Mpya ya Masoko

Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la Vision For Youth Vaileth Ayoub akitoa maelezo juu ya Mradi wa Soko Mkononi, Picha na Woinde Shiza

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Zaidi ya Wafanyabiashara 2000 wataweza kunufaika na Mradi wa soko mkononi unaotoa taarifa za masoko na uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki.

Kutokana na Changamoto ya Wafanyabiashara wa kati na wa wadogo kutokupata masoko mradi huo ulioko chini ya Shirika lisilikoua la kiserikali la Vision for Youth umeanza kutoa taarifa za masoko na fursa za uwekezaji.

Mkurugenzi wa Shirika hilo Violeth Ayoub alisema kuwa wanalenga nchi za Afrika Mashariki ila kwa sasa wameanza na Tanzania na Uganda ambapo kuna fursa nyingi za masoko na uwekezaji ambazo hazijatumika huwezi kulinganisha na Kenya ukiangalia hata uchumi wake umekua.

“Tumewalenga Wanawake na Vijana kuelewa fursa zilizopo na kuzitumia vizuri kubadilisha maisha yao na kufanikiwa kiuchumi” Alisema Vaileth

Mradi unatekelezwa kwa njia tatu ikiwemo kuwa na kituo cha cha taarifa juu ya namna ya kuingiza bidhaa ndani ya nchi na namna kupeleka bidhaa zako nje ya nchi ,sera za masuala ya biashara .

Mratibu wa Mradi huo Janeth Nyambo anaeleza kuwa kwa sasa dunia imekua kama kijiji unaweza kutumia simu yako ya mkononi kujua utawezaje kupata masoko ya biashara yako ,unaweza kuwekeza wapi badala ya kugombania fursa chache zilizopo.

Janeth Alisema kuwa kwa wale Wabunifu walioko Tanzania wanaweza kubuni kitu ambacho hakipo Uganda na wakapata fursa ya kukitangaza kupitia soko mkononi.