Waepuke Matapeli Hawa Wanaoitumia TGNP

Bango linaloonesha ofisi za TGNP


Waepuke Matapeli Hawa Wanaoitumia TGNP

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unapenda kuutangazia umma kuwa kuna mtu anayejiita Lilian Dihalo, mwenye namba za simu 0717-196386 na Email liliandihalo@gmail.com anayetuma ujumbe mfupi wa simu kwa watu mbalimbali kuwa kuna nafasi ya kazi ya Mhasibu Msaidizi imetangazwa na TGNP, na kumtaka muhusika atume fedha ili apatiwe ajira. TGNP haijatangaza nafasi za kazi kwa mwaka huu 2013 na Tangazo lolote la TGNP litakaloonekana kwenye mtandao wa www.zoomtanzania.com ni batili. TGNP hatuajiri kwa upendeleo au kupigiana simu kwa kupeana rushwa! Mtu yeyote atakae pokea Ujumbe wa aina hiyo afike ofisini kwetu Mabibo Dar es salaam, kudhibitisha kabla ya kufanya lolote. Tukio hili limeripotiwa Kituo cha Polisi Urafiki. URF/RB/673/2013

Tangazo limetolewa na Utawala TGNP!