Washindi wa shindano la Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling (kushoto) na Mwenzake Mark wakitembezwa na
kuangalia namna walemavu wa kituo cha Shanga River House cha jijini Arusha, washindi hao waliopatikana kupitia kampuni ya My Destination walikuwa nchini na kutembelea vivituo mbalimbali vya utalii na kukagua miradi mbalimbali kama hiyo.

Mshindi wa shindano la Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling akipuliza kioo kilicho yeyushwa tayari kwa
kutengenezwa chombo chochote ambavyo hutokana na taka ngumu zinazozalishwa na binadamu ikiwa ni moja ya shughuli zinazo fanywa na walemavu katika kituo cha shanga river house cha jijini Arusha.
kutengenezwa chombo chochote ambavyo hutokana na taka ngumu zinazozalishwa na binadamu ikiwa ni moja ya shughuli zinazo fanywa na walemavu katika kituo cha shanga river house cha jijini Arusha.
Allex na Mark wakipewa maelezo ya shughuli za kituo.
WADAU mbalimbali wa utalii wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kuutangaza utalii wa Tanzania katika maeneo yao ili kuwavutia watalii wengine kuzidi kufika kwa wingi hapa nchini kujionea maliasili zilizopo na kuchangia pato la taifa kwa ujumla.
Hayo yalielezwa jana na Ofisa Mtendaji wa TATO, Sirili Akko wakati akizungumza na wadau wa maswala ya utalii waliohudhuria katika hafla ya kuwapongeza vijana wawili walioshinda shindano lililoandaliwa na kampuni ya My Destination lililoshirikisha washiriki 122 ulimwenguni.
Aidha alisema kuwa, Tanzania ni nchi ambayo imebahatika kupata vivutio mbalimbali vya utalii hivyo kuwavutia watalii kufika na kujionea maliasili zetu, hivyo hawana budi kuutangaza utalii wetu katika nchi zao ili kuendelea kukuza utalii zaidi kwa nchi za Afrika.
Alisema kuwa, shindano hilo lilihusu mshiriki kuchagua vitu ambavyo wangependa kufanya maishani kabla
hawajafa ndipo vijana hao wawili waliposhiriki katika shindano hilo na kuoanisha kuwa wao wangependa kutembea dunia nzima na kujionea maajabu yaliyopo katika vituo mbalimbali.
hawajafa ndipo vijana hao wawili waliposhiriki katika shindano hilo na kuoanisha kuwa wao wangependa kutembea dunia nzima na kujionea maajabu yaliyopo katika vituo mbalimbali.
‘baada ya vijana hao kushiriki shindano hilo walishinda na kupewa nafasi ya kuchagua kutembelea nchi 25 kati ya 80 ambazo katika hizo nchi 25 walichagua nchi tatu za Afrika ikiwemo kutembelea Tanzania, Zimbabwe, na Afrika ya kusini na ndo maana wapo hapa leo tayari kwa kuanza zoezi hilo’alisema Akko.
Aliongeza kuwa, kitendo cha wao kuchagua Tanzania kati ya nchi 25 kimewafariji sana wao kama wadau wa utalii kwani imeonyesha jinsi ambavyo utalii wa nchi yetu unaweza kutangazwa na watalii mbalimbali na hatimaye kuweza kupata wageni wengi zaidi kwa kujionea maliasili zilizopo katika maeneo yetu.
Nao vijana hao walioshinda shindano hilo kutoka Calfonia Alex Ayling na Mark Ayling walisema kuwa, shindano hilo waliweza kushinda baada ya kukithi viwango vya shindano hilo na hatimaye wamefurahia sana kushinda kwani mchuano uliwashirikisha watu mbalimbali ulimwenguni.
Alex alisema kuwa, lengo la kuchagua Tanzania miongoni mwa nchi tatu za Afrika ambazo wangependa kutembelea
ni kutokana na uoto wa asili uliopo katika maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya kujionea wanyama mbalimbali kama sehemu ya uchaguzi wao.
ni kutokana na uoto wa asili uliopo katika maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya kujionea wanyama mbalimbali kama sehemu ya uchaguzi wao.
Alisema kuwa, katika maeneo hayo yote watakayotembelea watakuwa wakichukua mikanda mbalimbali kwa ajili ya kuirusha kwenye mtandao na hatimaye watu mbalimbali kuweza kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika vituo watakavyotembelea.
Mark alisema kuwa, wamekuwa wakifuatilia vitu mbalimbali vinavyoendelea Tanzania ikiwemo wanyama
mbalimbali wa kuvutia, pamoja na kufuatilia makabila ya wamasai ambayo watakuwa na nafasi ya kuwatembelea na kuweza kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwao.
mbalimbali wa kuvutia, pamoja na kufuatilia makabila ya wamasai ambayo watakuwa na nafasi ya kuwatembelea na kuweza kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwao.
walipewa zawadi na marafiki mbalimbali.