
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya jamii, Mhe. Azzan Zungu akifungua kikao na kuwakaribisha wadau wa elimu waliofika katika mkutano huo ili kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu bajeti ya elimu ya mwaka 2017/18.
Picha ya pamoja ya wadau wa elimu Tanzania na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge, huduma na Maendeleo ya Jamii baada ya kikao cha kuwasilisha mapendekezo ya wadau wa elimu katika bajeti ya elimu ya mwaka wa fedha 2017/2018 uliofanyika katika ukumbi mdogo wa bunge mjini Dodoma. Baada ya Kikao hicho wanakamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya jamii waliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa elimu ili kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini Tanzania.
husika ijikite katika maboresho ya mafunzo kwa vitendo kazi (Internship), mafunzo ya ufundi stadi na kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Pia aliiomba kamati hiyo kutoa pendekezo kwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo kuweka utaratibu thabiti na endelevu wa Kukusanya fedha za mikopo kwa wanufaika waliokwisha nufaika na mikopo hiyo ilikuongeza Wigo wa kuwapa mikopo wanafunzi wapya wa vyuo vikuu nchini. Pia tunaiomba serekali Ilitazame upya suala la ukusanyaji wa madeni ya walionufaika na mikopo, kubadilisha ghaflaMakusanyo toka asilimia nane (8%) hadi asilimia kumi na tano(15%) ni kuvunja mkataba wa mkopaji na mkopeshaji, jambo hili linavunja sharia. Kama ni lazima kufanya hivyo basi makusanyo hayo ya asilimia kumi na tano (15%) yaanzie kwa hawa wanaokopeshwa sasa ili wakope wakiwa wanalijua hilo.