Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa ambao ni waandaaji wa onesho alisema waliamua kufanya onesho hilo ili kutoa fursa kwa wananchi hasa wanaoelekea kufanya harusi kujua mitindo mbalimbali ya mavazi ambayo wanaweza wakaitumia katika shughuli zao za harusi na kuonekana tofauti kimuonekano.WABUNIFU wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi wamejitokeza kufanya maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi katika uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi ‘Precious Wedding House’ lililozinduliwa jijini Dar es Salaa. Uzinduzi huo uliofanyika jana eneo la Sinza Madukani ulipambwa na mbunifu wa mitindo kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kwa jina la Femi, mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania.
Alisema wabunifu walifanya maonesho ya mavazi katika mitindo mbalimbali kutumia mavazi ya hali zote ikiwa ni kuonesha jamii harusi si lazima muhusika au maharusi kutumia gharama kubwa bali wanaweza kutumia gharama za chini na kuonekana wenye mvuto kama watapata ushauri kutoka kwa wabunifu na wanamitindo.
Mbunifu maarufu wa mitindo kutoka nchini Nigeria, Femi (wa pili kushoto), pamoja na mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano (wa kwanza kulia) wakiwa katika pozi pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania, kwenye maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanyika katika duka la mavazi ya maharusi ‘Precious Wedding House’ lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.
|
Alisema duka lao pamoja na kuuza nguo za maharusi watakuwa wakitoa ushauri bure kwa maharusi endapo watafika katika duka hilo ambalo limekuja kuleta mabadiliko katika mitindo ya maharusi. Alisema duka hilo litahudumia watu wenye kipato cha chini, cha kati na hata cha juu kulingana na mahitaji ya wahusika huku wakinufaika kwa ushauri bure kila atakaetembelea na kuomba ushauri kwa wataalamu wa mitindo.
Alisema duka hilo kubwa la mitindo ya maharusi wa kike na kiume linatumia wataalamu wa mitindo kutoka nchi za Uturuki, Marekani, Italia pamoja na Tanzania. Alisema wamekuja kuondoa dhana iliyojengeka kuwa nguo za maharusi ni anasa kutoka na maduka mengi kuuza bei kubwa kuliko inavyotegemewa, hivyo kupitia kwa wataalam wao maharusi wanaweza kufanya shughuli kwa bei ndogo na kuvutia.
“…Watu wengi wanaona mavazi ya maharusi ni kama anasa kutokana na bei kubwa za mavazi haya, sisi tumeamua kuleta mabadiliko hapa dukani kuna nguo za makundi yote, yaani watu wa kipato cha chini, watu wa kipato cha kati na hata watu wa kipato cha juu…unaweza kuandaliwa nguo yako ya harusi na wanamitindo kutoka nchi tulizotaja wewe ukiwa hapa hapa nchini na ukaipata ndani ya siku 21.
Akizinduwa duka hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang, Emelda Mwamanga alimpongeza mwanamama mjasiliamali na mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo kwa uamuzi wa kusaidia kutoa ushauri kwa maharusi jambo ambalo limekuwa likipasua vichwa kwa wahusika. Alisema kitendo hicho kinatoa changamoto kwa akinamama wajasiliamali kuweza kufanya mambo
makubwa kibiashara.
Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kulia) akigonganisha glasi ya mvinyo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo. |