Wabunge Ujerumani wamgomea Pope Benedict XVI! Watoka bungeni

Heti siasa na dini ni sawa kuchanganya maji na mafuta katika chupa?
Wengine wanadai kisa kupingwa kwa kondomu! Kweli Nabii hana utukufu nyumbani kwao !?

KIONGOZI wa kidini wa kanisa la Kikatoliki duniani Mtakatifu Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger), amejikuta yupo katika mvutano mkubwa na wanasiasa nchini ujerumani, baadhi wabunge wapatao 100
wametoka nje ya bunge la ujerumani wakati Pope Benedict akiwa analihutubia bunge la nchi hiyo (Bundestag) majira ya halasiri ya alhamisi 22-09-2011 mjini Berlin, ambako Baba mtakatifu
yupo ziarani nchini ujerumani!

Wabunge hao wamemsusia Pope na kutoka nje ya bunge ambako walijumuhika na waandamaji wa wengine waliokuwa wanampinga Pope kuwepo katika ukumbi wa bunge hilo!
Habari za uhakika zinaeleza kuwa baadhi ya wanasiasa na wabunge nchini ujerumani hawakubaliani na taratibu za uongozi wa Pope, haswa linapokuja swala la matumizi ya KONDOMU, kwani kanisa la kikatoliki halikubaliani na matumizi ya kondomu, pia sababu zingine za kupingwa kwa Pope nchini ujerumani ni pamoja kashifa zinazowagusa baadhi ya watumishi wa kanisa la kikatoliki duniani kwa kuhusika na kuwafanyia vitendo vichafu watoto au vijana katika miaka ya nyuma.

Pope Benedict amekuwa muwazi na amewahi mara nyingi kuomba radhi hadharani kwa niaba ya kanisa lake, lakini wakosoaji bado wanaendeleza nongwa ! sababu nyingine ya wanaopinga kulihutubia bunge la Ujerumani ni kuwa DINI NA SIASA ni vitu viwili tofouti kwa maana hii Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger) hapaswi kuhuwepo ndani ya jumba au kulihutubia bunge ambalo ndilo baraza la kutunga sheria.
Pope Benedict xvi ni mzaliwa wa ujerumani,alizaliwa kwa jina la Joseph Ratzinger, huko Bayern, Ujerumani ya kusini. Vyombo vya habari nchini ujerumani vimetonya kuwa kuanzia mwaka 2010 wafuasi wapatao 160,000 wa kanisa la kikatoliki nchini Ujerumani wamelihama kanisa hilo na kujiunga na madhehebu mengine.