![Ziara ya Wabunge wa CHADEMA Washington DC](http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/05/DSC8668.jpg)
Baada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha Tawi la CHADEMA Washington DC Maryland na Virginia, Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa na Nassari Joshua, a.k.a 'Dogo Janja', Usiku wa jana Jumatano Mei 30, 2011 waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland nchini Marekani.
![Wabunge wa CHADEMA washuhudia mpambano wa kimataifa](http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/05/DSC8913.jpg)
Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa na Nassari Joshua, maarufu 'Dogo janja' wakiwa na uwongozi wa Tawi la CHADEMA Washington DC, Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla, Aboh Shatry (wa pili kulia), pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa. (Picha zote na swahilivilla Blogu)