Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wala Kiapo

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo

Samuel Sitta ni muwakilishi wa Tanzania

Charles Makongoro Nyerere

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.
Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.
Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose SaddrudinBhanji.
Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.
Wabunge hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na