Wabunge EALA Watembelea Taasisi ya Sanaa, Utamaduni Bagamoyo

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonesha na kuuza bidhaa zao  wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo.

Mbunge wa  Bunge  la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Margareth Zziwa mara baada ya kuvutiwa na bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), Margareth Zziwa (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), Margareth Zziwa akipanda mti katika eneo la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira. Picha zote na Frank Shija - Maelezo.

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), Margareth Zziwa akipanda mti katika eneo la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira. Picha zote na Frank Shija – Maelezo.

Na Eleuteri Mangi – MAELEZO

WABUNGE wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Dk. Margaret Zziwa wametembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kujionea vitu mbalimbali vilivyomo ndani ya taasisi hiyo ya mjini Bagamoyo.

Spika wa Bunge la EALA, Dk. Zziwa pia alipewa heshima ya kupanda mti aina ya mtiki ikiwa ni ishara ya kuthamini, kuhifadhi na kutunza mazingira nchini. Spika Dk. Zziwa ualipanda mti huo wakati wa ziara yake pamoja na wabunge wa EALA walipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana mjini Bagamoyo.

“Huu ni utaratibu wetu na ni azimio tuliojiwekea kama EALA kupanda miti kila tunapoenda kufanya mkutano katika nchi washirika ndani ya jumuiya yetu ili kuwasisitiza wananchi umuhimu wa kutunza mazingira,” alisema Dk. Zziwa.

Dk. Zziwa alisema kuwa imekuwa desturi ambayo pia ni utaratibu waliojiwekea bunge hilo kupanda miti kila wanapokuwa na mkutano kila mwaka katika nchi washirika ambapo mikutano hiyo hufanyika kwa mzunguko ndani ya jumuiya.

Dk. Zziwa alieleza kuwa zoezi la kupanda miti hiyo lilikuwa lifanyike Dar es Salaam lakini yeye na wabunge wa EALA waliamua lifanyike Bagamoyo ambapo pamoja na kutembelea Taasisi ya TaSUBa wamepata kujionea hazina ya historia Afrika Mashariki iliyopo katika Mji Mkongwe wa Bagamoyo.

Aidha, Dk. Zziwa amempa jukumu la Mbunge wa EALA kutoka Tanzania ShyRose Bhanji kutembelea taasisi hiyo na kujionea hali ya miti waliyoipanda wakati wa ziara yao inavyoendelea kumea na kutoa taarifa mara kwa mara katika bunge hilo. Kwa upande wake Mbunge wa EALA kutoka Tanzania Makongoro Nyerere ametoa wito kwa Watanzania wa kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi iwezekanavyo ili kutunza mazingira.

Makongoro amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi ahamasike, kila mwananchi mmoja mmoja apande mti mmoja autunze hadi ukue. Makongoro alisisitiza kwa kusema, “Miti ina umuhimu mkubwa sana katika jamii yetu, inasaidia kutunza uso wa ardhi yetu na rutuba kwa manufaa ya kilimo bora katika nchi yetu”.

“Miti ni uchumi katika nchi, inatumika kujengea, kutengenezea samani za maofisini na majumbani, viwandani kutengeneza vitu mbalimbali ikiwamo viberiti na vyombo vya kusafiria vya baharini,” alisema Makongoro.

Aidha, Makongoro alisema kuwa kutokana na hatari ya mabadiliko hali ya tabia nchi yanavyoendelea, ni wajibu wa kila Mtanzania kutunza mazingira na kuzingatia usemi wa “Kata mti, Panda miti,” ili kuboresha hali ya hewa nchini na mazingira yawe rafiki kwa viumbe vyote vilivyopo kwenye maji na nchi kavu wakiwemo wanyama, mimea, samaki na viumbe wengine wanaoishi kwenye maji.

Katika tukio la upandaji miti, ilipandwa jumla ya miti mitatu katika taasisi ya TaSUBa ikiwa ni juhudi zinazofanywa na bunge la EALA katika kutunza mazingira kwa vitendo. Mti wa pili ulipandwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara na wa tatu ulipandwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki, Dk. Abdala Juma Abdulla Saadalla.