Wabunge EAC Tanzania waomba kutangazwa na wanahabari

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Tasilimu akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambao wataufanyia kazi katika kikao cha Bunge kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao walizungumza na waandishi wa habari.

Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania, Shy-Rose Banji (kushoto) akiwaomba waandishi wa habari watangaze umuhimu wa Bunge hilo na fursa zilizopo kwa wajasiriamali hasa wanawake. Wabunge hao wamezungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo). Katikati ni Mwenyekiti, Adam Kimbisa akifuatiwa na Angela Kiziga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira. (Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo)