WAASI katika Jimbo la Kordofan Kusini, nchini Sudan wamesema kuwa wametungua ndege ya kijeshi karibu na mpaka wake na Sudan Kusini. Msemaji wa kundi la SPLM-North alisema kuwa ndege hiyo ilitunguliwa kufuatia ufyatuaji mkubwa wa risasi katika eneo la milimani la Nuba siku ya Jumatano.
Hakuna tamko lolote kutoka kwa serikali ya Khartoum kuhusu shambulizi hilo. Waasi wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Sudan katika eneo hilo tangu Juni mwaka jana. Mzozo huu wa Kordofan Kusini pamoja na Ule wa jimbo la Blue Nile umewafanya maelfu ya watu kutoroka makwao.
-BBC