Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Wakutana na Mwenyekiti wa NEC.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini NEC imewataka waangalilizi wa uchaguzi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ya waangalizi wa uchaguzi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu.

Hayo yaliyasemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji mstaafu Damian Lubuva alipokuwa akizungumza na waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka nchi za Jumuiya ya Madola uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

“Tunataka amani na utulivu wa nchi uendelee kuwepo hata baada ya uchaguzi hivyo fanyeni kazi yenu ya uangalizi kwa kuzingatia sheria na msikiuke misingi ya sheria hiyo”,alisema Jaji Lubuva.

Akizungumza kuhusu maswali waliyomuhoji waangalizi hao Jaji Lubuva alisema waangaliza hao walizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo maandalizi ya uchaguzi kwa upande wa Tume ikiwa ni pamoja na usambazaji wa vifaa, ambavyo vimekwisha sambaazwa nchi nzima.

Mbali na hayo Mwenyekiti wa NEC alitoa ufafanuzi kwa waangalizi hao wa uchaguzi katika suala la wapiga kura kutosimama hata baada ya mita 200 katika vituo vya kupiga kura.

“Tume iliamua kutoa tamko hilo baada ya kuona changamoto za wapiga kura na kuamua kutoa maelekezo kuwa watu wakishapiga kura waondoke vituoni wakaendelee na shughuli zao,lakini hata hivyo kwasasa suala liko mahamamani lakini msimamo wa Tume ni ule ule kwani mikusanyiko hiyo huweza kuchangia uvunjifu wa amani ila tataendelea kusikiliza mahakama itaamua nini” aliongeza Jaji Lubuva.

Aidha Tume imesema uchanguzi unaonekana kufuatiliwa na wananchi wengi na wito wake kwa wananchi hao ni kwenda kupiga kura huku wakilinda amani na utulivu wan chi A kwa kuondoka katika kituo cha kupiga kura na kwenda kuendelea na shuguli zao na kuwataka warudi vituoni jioni kuangalia matokeo.

Hata hivyo tume imewataka viongozi wadini waendelee kuhubiri amani kwa waumini wake na kuwasihi viongozi wa vyama waache kuwaambia wafuasi wao wabaki vituoni mara baaada ya kupiga kura kwani mikusanyiko hiyo huweza kuchangia uvunjifu wa amani.