Mkutano huu uliowakutanisha pamoja waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) umeratibiwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo.
Mtaalam wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro akielezea kwa ufupi jinsi Umoja wa Mataifa unavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na kufafanua Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumzia yatokanayo mkutano wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo swala la Gesi joto ambapo amesema kwa nchi kama Tanzania haichafui mazingira kulinganisha na nchi zinazoendelea zenye viwanda vikubwa pamoja na makubaliano waliyofikikia katika mkutano huo ambayo yatatolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira hivi karibuni.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari za Mazingira (JET) wakiuliza maswali na kutoa maoni kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (hayupo pichani).
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya waandishi wa habari wa Mazingira (JET) waliohudhuria mkutano huo.
Afisa habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma akitoa changamoto kwa waandishi wa habari wa mazingira kuzipa kipaumbele habari za mazingira na kuwataka kuweka usawa katika habari wanazoandika.