Waandishi wa habari ‘wasaka’ almasi Songwa

Baadhi ya waandishi wa habari wakijaribu kutafuta ishara za madini ya almasi Mji mdogo wa Songwa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga yalipo machimbo ya almasi

Baadhi ya waandishi wa habari hao wakipiga picha na baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliofanya mahojiano mbalimbali na wanahabari.

Baadhi ya waandishi wa habari hao wakipiga picha na baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliofanya mahojiano mbalimbali na wanahabari.

Na hapa ndipo alipo muwekezaji mkubwa wa madini ya almasi anayeendesha shughuli zake eneo la Mwandui.

Hapa tukipata picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari wa mkoani Shinyanga katika ofisi yao ya mkoa (Shinyanga Press Club)

Kazi na dawa! Baadhi ya wanahabari hao wakiponza tumbo eneo la Mwandui walipokuwa kazini katika mahojiano na wananchi.

Waandishi wanaofanya habari za uchunguzi maeneo ya vijijini Kata ya Songwa, Wilaya ya Kishapu mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza warsha ya siku mbili iliyoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kabla ya kuingia kazini.

Na Mwandishi wa dev.kisakuzi.com, Songwa-Shinyanga

BAADHI
ya waandishi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoani Shinyanga wametembelea machimbo ya almasi yanayofanywa na wananchi eneo la mjini mdogo wa Songwa.
Ziara ya waandishi hao imekwenda sambamba na kufanya uchunguzi juu ya huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na Serikali kwa wakazi wa maeneo hayo, yaliomo ndani ya Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.
Waandishi hao wameshuhudia namna wananchi na hasa vijana wanavyojishughulisha na shughuli nzima za machimbo ya madini ya almasi licha ya Kata ya Songwe kukabiliwa na huduma duni za maji safi na salama kwa matumizi yao pamoja na yale ya shughuli za machimbo.
Mtandao huu utawaletea mahojiano ya wananchi eneo hilo pamoja na hali halisi ya huduma anuai za kijamii kwa wakazi wa Kata hiyo ya Songwa iliyopo Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga muda si mrefu.