Waandishi Tanzania Waadhimisha Kuzaliwa kwa Mzee Mandela

Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya hafla fupi ya kuzaliwa Mzee Mandela

Ofisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari- MAELEZO, Anna Itenda akitoa maelezo mafupi jinsi alivyofanya kazi na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela pamoja Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa idara hiyo, Zamaradi Kawawa. Picha zote – Hassan Silayo – Maelezo.

Ofisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari- MAELEZO, Anna Itenda akimlisha  keki Afisa Habari Mwandamizi wa idara hiyo, Jovina Bujulu wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, huku waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifurahia hafla hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO.

Ofisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari- MAELEZO, Anna Itenda akikata keki  wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee  Nelson. Keki hiyo iliandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO.