Waandamanaji Bukina faso Wachoma Bunge Kumpinga Rais

Baadhi ya magari na majengo yakiteketea kwa moto baada ya waandamanaji kuchoma.

Baadhi ya magari na majengo  ya Bunge la nchi ya Bukina Faso yakiteketea kwa moto baada ya waandamanaji kuchoma.

Wananchi wakionesha asira zao kwenye maandamano.

Wananchi wakionesha asira zao kwenye maandamano jirani na majengo ya bunge la nchi hiyo.

Rais Blaise Compaore

Rais Blaise Compaore

Wananchi wakiandamana.

Wananchi wakiandamana.

WANANCHI wa Bukina Faso wanaoendeleza maandamano wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, ikiwa ni hatua ya kupinga kuongeza muhula wa kutawala kwa Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo ambaye ametawala nchi kwa miaka 27.

Vituo vya Televisheni ya Taifa navyo vililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji hao kuvamia majengo ya shirika la utangazaji. Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais huku wanajeshi wakijaribu kuwafyatulia risasi.

Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa kwa moto. Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa. Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubali, Compaore kuwania tena Urais kwa mwaka ujao.

Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa makubwa zaidi kuukumba utawala wa Rais Blaise Compaore. Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.

Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987. Amekua akishinda uchaguzi lakini ushindi wake wa kura hugubikwa na utata mara zote. Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena urais ili kuzuia machafuko na kutoa demokrasia kwa wengine.
-BBC