SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) kwa kupitia Chama cha Waamuzi wa Ngumi za Ridhaa wameteua na kuwathibitisha waamuzi watakao tumika katika mashindano ya ubingwa wa taifa yatakayofanyika kuanzia Septemba 17 hadi 22, 2012 uwanja wa taifa wa ndani.
Kwa mujibu wa taarifa yao kwa vyombo vya habari waamuzi waliopitishwa ni pamoja na Mohamed Kasilamatwi mwamuzi wa kimataifa na Juma Selemani mwamuzi wa Afrika kama wasimamizi wa waamuzi.
Waamuzi wa ngazi ya taifa walioteuliwa ni Maneno Omari, Ridhaa Kimweli, Mohamed Bamtulla, Shija Masanja, Mafuru Mafuru, Moshi Makali, Hamza Abdallah na Marko Mwankenja.
MAKORE MASHAGA (KATIBU BFT) 0713588818