
Lile Tamasha la Kiafrika mjini Tuebingen, Ujerumani lafanyika tena kuanzia tarehe 23 – 26 mwezi huu (leo mwisho) na kukonga nyoyo sio tu za Wajerumani, na wageni wengine, bali pia na Waafrika wenyewe. Pichani ni bango maalum la tamasha hilo.

Wazungu wakiwa wanakandamiza misosi ya Kiafrika kabla ya kuanza kuona show.

Muafrika akiwa jukwaani kutoa burudani ya nguvu, ambayo ilihusisha uzungushaji wa masinia kadhaa kwa miti kama uonanvyo hapo.

….Burudani ya masinia ikiendelea…

Muda wa kupagawisha watoto uliwadia, na watoto wote wakaitwa jukwaani…weupe, wekundu, weusi… almuradi ni kufurahi tu!

Huyu jamaa, ambaye TheHabari haikuweza kupata jina lake mara moja, alifurahisha sana wototo….wa rangi zote.
Picha na Habari zote zimeletwa na Mwakilishi wa Thehabari, Tuebingen, Ujerumani